Friday, September 14, 2012

KILICHOAFIKIWA NA WAANDISHI WA HABARI KWENYE MAANDAMANO SEPT 11 DAR ES SALAAM.


Haya ni maandamano ya waandishi wa habari Mwanza.
Jukwaa la Wahariri Tanzania pamoja na waandishi wa habari waliungana na kufanya maandamano kuanzia mkao makuu ya kituo cha Television cha Channel Ten mpaka kwenye viwanja vya Jangwani Dar es salaam september 11 kupinga mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi alieuwawa kwa kulipukiwa na bomu akiwa mikononi mwa polisi Iringa wakati polisi walipokua wakiwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo.
Mjumbe wa jukwaa la wahariri kutoka Zanzibar Masoud Sanani kwenye maandamano hayo Jangwani  alitangaza maazimio yaliyofikiwa na washiriki wa maandamano hayo, namkariri akisema “kwa siku 40 hizi za maombolezo tusiandike habari ya polisi, polisi hata akifanya kitu gani tusiandike, wataandika kwenye gazeti lao la polisi wanalo”
.
Katibu wa jukwaa la wahariri Tanzania Neville Meena alizungumza pia na kuamplfy kwamba vyombo vya habari vinafanya kazi kubwa kwa kufuata taaluma na havipo kwa ajili ya maslahi ya mtu yoyote.
Namkariri akisema “sheria zetu ni kandamizi sana ndio maana leo hii tunahangaika, Wakuu wa Polisi Iringa na wenzie waliohusika na lile jambo ambao ushahidi uonyesha kabisa kwamba kuna kuhusika kwa polisi wamekaa kimya mpaka leo, hatujasikia polisi wanasema jambo lolote mpaka leo, kwa sababu sheria zetu zimekaa vibaya kwa hiyo jitihada za kuhakikisha tunapata sheria mpya za habari tuendelee nazo tupate sheria mpya ili mwisho wa siku tuhakikishe tunakua na maisha salama”
Waandishi wa habari Mwanza picha zimepigwa na Albert G Sengo wa gsengo.blogspot.com
Kwenye line nyingine ni kwamba waandishi hao wa habari walioandamana walilazimika kupinga ujio wa Waziri wa mambo ya ndani Dr Emmanuel Nchimbi aliehudhuria maandamano hayo Jangwani ambapo waandishi walisikika wakisema “maandamano haya ni ya waandishi na wahariri wetu kwa hiyo Nchimbi aondoke”
Baada ya hapo sauti kupitia kipaza sauti ilisikika ikisema “kwa sababu mmesema, tukampelekea ujumbe Mh Waziri hawa jamaa wanasema tupishe, tunakuomba gari yako iko pale taratibu tunaomba uondoke, amewaona akaamua aondoke… hatuna ugomvi na serikali wala hatuna ugomvi na wizara yoyote ile ila shughuli ya leo imemkataa na tunaomba salamu zetu zimfikie kwamba tunampenda sana, ni rafiki yetu ni waziri wetu lakini hakuwa na vazi la msiba”

1 comment:

  1. eToro is the ultimate forex trading platform for rookie and established traders.

    ReplyDelete

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...