Sunday, September 9, 2012

Scotland na Serbia zatoka sare


Scotland na Serbia zikimenyana Sept 8
Timu za Scotland na Serbia ziliumiza nyasi bure siku ya Jumamosi kwani walitoka sare ya bila-kwa-bila katika mechi ya kuwania nafasi ya kucheza katika fainali za kombe la dunia , nchini Brazil mwaka 2014.
Mechi nzima pia ilikosa msisimko katika dakika zote 90 huku timu hizo kionekana kutokuwa na mbinu zozote.
Linalokumbukwa katika mechi hiyo iliyochezwa Scotland ni kwamba katika dakika za awali kipa Allan McGregor aliokoa kombora kutoka kwa mshambulizi wa Serbia Aleksandar Kolarov. Na kipa huyo wa Scotland pia aliokoa mkwaju toka kwa Dusan Tadic katika dakika za mwisho.
Lakini kijumla mechi nzima ilikosa msisimko.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...