Wednesday, September 26, 2012

SAJENT AMSHUKIA NAY WA MITEGOSTAA wa filamu Bongo, Husna Idd ‘Sajent’ amemvaa mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki  ‘Nay wa Mitego’ na kusema wimbo wake uliolenga kuwachafua Bongo Movies, ulipaswa uwe wa wanamuziki na si wao.
Akizungumza na Tollywood Newz, Sajent alisema amesikitishwa na wimbo wa Nay uitwao Nasema Nao ambao ndani yake kuna mashairi ya kuwaponda wasanii wa filamu kuwa ndiyo wanaoongoza kwa umalaya.
“Hata siku moja nyani hajawahi kuona makalio yake, yeye ataendelea kuwacheka wenzake kuwa wana makalio mekundu, lakini hajayaona yake.
“Ni sawa na Nay sasa. Yeye ni mropokaji, anatafuta njia ya kujipaisha kisanii. Sasa jamani, hivi sisi wa filamu na wao (Bongo Fleva)  ni akina nani wanaongoza kwa umalaya? Atasema sana, lakini ukweli utabaki palepale na huyo Nay mwenyewe anauja ukweli.”

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...