Wednesday, September 26, 2012

FLORA, H. BABA PENZI MOTOMOTOWAPENZI mastaa wa filamu na muziki Bongo, Flora Mvungi na Hamis Baba ‘H. Baba’ wamewakata vilimi watu wanaochonga ili kuwagombanisha ambapo H. Baba amefunguka: “Watasubiri sana, hapa ni penzi motomoto.”
H. Baba alisema hayo wikiendi iliyopita aliponaswa na kamera yetu wakiwa wamegandana na Flora pande za Leaders Club, Kinondoni, Dar.
“Yanasemwa mengi kuhusu penzi letu, lakini mimi naweka wazi hakuna wa kutugombanisha kwani tumetoka mbali. Tumeshafikia malengo mazuri, kilichobaki sasa ni ndoa,” alisema H. Baba.
Awali paparazi wetu alipowaona wawili hao wamejitenga na eneo lenye watu wengi huku wakiwa wameshikana kimahaba, fasta aliwafotoa picha kisha akawasogelea ili kupata habari kamili, akagundua walikuwa ni H. Baba na Flora.
Kwa upande wa Flora alisema: “Watuache sasa jamani, tumeshawachoka. Najua wengi wanaumizwa lakini labda niwasaidie kwa kuwaambia waangalie ustaarabu mwingine kwani maisha yetu hayatawasaidia chochote.”

1 comment:

 1. It is perfect timе to make sοmе рlans for the long гun аnd it is tіme
  to be happy. I havе reаd thіs publіsh anԁ іf І may just I wish tο suggеѕt you
  ѕome аttention-grabbіng iѕsues or suggestions.
  Pеrhаpѕ you can wгitе subѕequent articles referrіng tо thіs aгticle.
  I wish to rеad mοre things approxіmately it!


  My ωeb-site - payday loans

  ReplyDelete

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...