Sunday, September 16, 2012

QPR yaizima Chelsea kwao


Chelsea 0-0 QPR

Anton Ferdinand akataa kumsalimia Terry
Timu ya Queen Park Rangers siku ya Jumamosi ilizima rekodi ya Chelsea ya kuzifunga timu tangu msimu wa ligi ya Uingereza ianze mwaka huu baada ya kutoka sare bila kufungana bao lolote.
Kwa sare hiyo QPR ilijizolea pointi mmoja katika ligi hiyo.
Hatua ya mlinzi Anton Ferdinand kukataa kumsalimia nahodha wa Chelsea John Terry kabla ya mechi kuanza ilifanya mechi hiyo kukosa msisimko.
Beki huyo wa QPR pia alikataa kumsalimia mlinzi wa Chelsea Ashley Cole .
Anton alikataa kumsalimia Terry kutokana na madai kwamba katika mechi yao ya msimu uliopita nahodha huyo wa Chelsea alimkejeli na kumtolea maneno ya ubaguzi wa rangi.
Wakati wa Kesi hiyo Cole alikuwa shahidi upande wa Terry.
Lakini mahakama ya Uingereza ilimpata Terry bila ya makosa wakati alipofunguliwa mashitaka.
Hata hivyo katika mechi hiyo ya Jumamosi,Chelsea walilalamika kuwa muamuzi aliwanyima nafasi za wazi mbili za kufunga kwa njia ya penalti.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...