Man U 4-0 Wigan
Licha ya umri wake ,Paul Scholes
alionyesha umahiri wa soka baada ya kuifungia Manchester United bao la
kwanza walipocheza na Wigan katika uwanja wa Old Trafford siku ya
Jumamosi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alifunga bao hilo dakika sita tu baada ya timu hizo mbili kutoka mapumzikoni.
Hii ilikuwa ni mechi ya 700 kwa Scholes kuichezea Man U .
Mchezaji Javier Hernandez ambaye mkwaju wake wa
penalti uliokolewa na Kipa wa Wigan Ali Al Habsi hapo awali, alifunga
katika dakika ya 63 kabla ya Alex Buttner na Nick Powell kufunga katika
dakika ya 66 na 83 hivyo mpira ukimalizika kwa mabao 4-0
Japo Man U walifunga lakini hawakuonyesha mchezo
mzuri ila tu walitumia nafasi chache walizozipata na kufunga mabao ya
haraka haraka.
Sasa vijana wa Sir Alex Ferguson wako katika
nafasi ya pili, pointi moja tu nyuma ya vinara Chalsea ambao walitoka
sare na timu ya Queen Park Rangers siku hiyo hiyo ya jumamosi.
No comments:
Post a Comment