Sunday, September 16, 2012

Arsenal yanyeshea Southampton

Arsenal 6-1 Southamton
Ni furaha baada ya kuipa Arsenal bao
Arsenal ilionyesha mchezo safi uliojaa mashambulizi na kuwafanya wapate mabao matatu katika dakika saba ya kipindi cha kwanza wa mechi kati yao na Southampton.
Jos Hooiveld wa Southampton aliipatia Arsenal bao la kwanza baada ya kujifunga mwenyewe kabla ya Lukas Podolski kuvurumisha mkwaju mkali toka umbali wa yadi 25 na kufanya mambo kuwa 2-0.
Kiungu Gervinho aliwapa vijana wa Arsene Wenger bao la tatu kabla ya Nathaniel Clyne wa Southampton kujifunga mwenyewe.
Hata hivyo Danny Fox alijitahidi na kuwapa wagine bao la kufutia machozi.
Baada ya kutoka mapumzikoni, mwamba Gervinho aliipa Arsenal bao la tano kabla ya Theo Walcott kufunga la sita mara tu baada ya kuingizwa uwanjani.
Licha ya kucheza mechi nne Southampton hadi sasa bado haijapata pointi yeyote na inavuta mkia katika ligi hiyo ya Uingereza.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...