Tuesday, September 11, 2012

MAADHIMISHO YA MIAKA 11 YA TUKIO LA UGAIDI NCHINI MAREKANI 'SEPT 11, 2001'

Mwanamama Rosario Tejada wa Columbia (kulia) akitafuta jina la mpwa wake aliyefariki katika tukio la kigaidi Septemba 11, 2001 leo katika Kituo cha Kimataifa cha Biashara (WTO) jijini New York . Pichani ni waombolezaji wengine waliohudhuria tukio hilo.
Maria Rodriguez akiomboleza pembeni ya picha za marehemu mkwe wake, Emilio Ortiz aliyefariki katika tukio la ugaidi la Septemba 11, jijini New York.
Kituo cha Kimataifa cha Biashara (WTO) kikiwaka moto baada ya kulipuliwa Septemba 11, 2001.
(Picha zote na AP)
MAMIA ya Wamarekani leo wameungana tena katika maadhimisho ya kumbukumbu za tukio la ugaidi lililotekea Septemba 11, 2001 katika majiji ya New York na Washington nchini Marekani.
Umati huo ulikusanyika katika maeneo ya Kituo cha Kimataifa cha Biashara (WTO) jijini New York na Makao Makuu ya Kijeshi ya Marekani, Pentagon kusoma majina ya watu zaidi ya 3,000 waliouawawa katika mashambulizi hayo.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...