Tuesday, September 11, 2012

SHILOLE ANASWA NA BWANA MPYA


MSANII wa filamu na muziki wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, juzikati alinaswa akiwa na bwana mpya aliyetambulika kwa jina moja la Ombeni wakila bata ndani ya Club ya Laca sachika jijini Tanga, siku moja kabla ya Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kufanyika ndani ya Viwanja vya Mkwakwani, Musa Mateja anashuka nayo.
Wawili hao walinaswa wakijiachia kwa raha zao huku wakionesha waziwazi kukolezana kimalavidavi ambapo baada ya kuwafotoa picha kadhaa, mwandishi wetu alitaka kufahamu ukweli wa uhusiano wao ambapo wote walikiri kuwa wanatoka kimapenzi.
“Kweli natoka na Shilole kimapenzi lakini naomba usiandike gazetini maana utaniharibia mambo yangu mengi kwa mabosi wangu,” alisema Ombeni huku Shilole naye akithibitisha suala hilo na kueleza kuwa walisafiri pamoja kutoka Dar, naye akaomba ishu hiyo isichorwe gazetini. Baada ya kujiachia kwa sana, wawili hao waliondoka na kwenda kulala pamoja.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...