Tuesday, September 11, 2012

EPIQ BONGO STAR SEARCH MSHIRIKI AMGANDA SALAMA AMPE KAZI YA UTANGAZAJI


Salama Jabir (kulia) akiwa na majaji wenzake Madam Rita na Master J.
ZOEZI la usaili wa washiriki wa Shindano la Epiq Bongo Star Search lililokamilika hivi karibuni, lilijaa vituko kibao ambapo mshiriki mmoja wa kiume kutoka Songea, alimganda Salama Jabir ambaye ni mmoja wa majaji wa shindano hilo, ampe kazi ya utangazaji kama yeye kwani anaamini ana kipaji kikubwa cha fani hiyo kuliko kuimba.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, mshiriki huyo alipewa nafasi ya kuonesha kipaji chake lakini badala ya kufanya hivyo, alianza kujinadi kwamba anaweza kutangaza vizuri na kumganda Salama ampe kazi.
“Mi kuimba siwezi vizuri ila naweza kutangaza redioni, nilianza kukuona Salama kwenye TV na kwenye magazeti namshukuru Mungu leo nimekuona live, hapa siondoki mpaka kieleweke, nataka unipe kazi ya utangazaji,” alisema mshiriki huyo, majaji wengine ikabidi waingilie kati na kumuahidi kuwa watamuunganisha na Salama. Hata hivyo, mshiriki huyo hakupata nafasi ya kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...