Tuesday, September 18, 2012

GARI LARUKA JUU, LAINGIA CHUMBANI GHOROFANI, SURREY, UINGEREZA


Wataalam wakiangalia shimo lililosababishwa na gari lililoruka juu huko  Epsom, Surrey, Uingereza.
MTU na mkewe waliokuwa wamelala eneo la Epsom, Surrey, Uingereza,  walishituka vibaya baada ya gari moja dogo ‘kuruka juu mita 24 (futi80)’ na kutua katika chumba walichokuwa wamelala.
Hii ilitokea majuzi wakati gari lenye rangi ya fedha aina ya Lexus lilipoigonga nyumba hiyo na kuharibu sehemu kubwa ya chumba hicho cha kulala ambapo polisi walisema kabla yake liliparamia gari aina ya Audi lililokuwa limeegeshwa.
Bahati nzuri, hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo lililotokea Barabara ya Bridge Road, wakiwemo watoto wawili waliokuwa wamelala chumba cha pili
.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...