Tuesday, September 18, 2012

RAIS WA URUSI ANAPOSHINDANA NA NDEGE KUPAA


Rais wa Urusi, Vladmir Putin akifanya mashindano ya kupaa angani kama ndege.
RAIS wa Urusi, Vladmir Putin hivi karibuni alifanya tukio liliwashangaza wengi, kufuatia kitendo chake cha kufanya mashindano ya kupaa angani kama ndege.
Putin, alitumia kishada kilichofungwa injini ya helikopta ambacho kilimuwezesha kupaa angani na akiwa juu, alishindana na ndege kukata upepo.
Rais huyo ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Umoja wa Urusi tangu mwaka 2008, siku hiyo ya mashindano yake na ndege, alivaa nguo nyeupe ili kufanana na ndege aina ya kongoro na kabla ya kupaa, alikuwa anazungumza maneno kama anawaambia ndege waanze mashindano.
Televisheni ya Urusi, ilirusha tukio hilo moja kwa moja kuanzia mwanzo alivyoanza kujiandaa kupaa, alipokuwa anazungumza na ndege mpaka alipotua.
Baada ya kutua, Putin alisema kuwa alilazimika kukatisha safari na kutua baada ya kuona chombo chake kinapepea kwa kasi angani, hivyo kumuashiria hatari mbele yake.
Katika safari hiyo, Putin alianza kupaa angani na ndege watano ambao walikuwa wakiongozana naye lakini baadaye walibaki wawili, baada ya watatu kushika kasi na kupotelea angani.
Safari hiyo iliwafurahisha wananchi wa Urusi na wengine waliamua kurusha picha za rais huyo akiwa angani kwenye mitandao mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...