Saturday, September 29, 2012

EXCLUSIVE: YOTE ALICHOSEMA GODBLESS LEMA KUHUSU VITISHO NA KESI YAKE


.
Hii post inamuhusu aliekua mbunge wa Arusha mjini kupitia CHADEMA Godbless Lema ambae alivuliwa ubunge na Mahakama.
Kuna mambo mengi niliyotamani kumuuliza kabla ya kukutana nae ambayo hata hivyo nilimuuliza na yote akayatolea ufafanuzi kwenye hii exclusive interview.
Kuhusu kupata vitisho, Lema amesema “kutishwa, kutukanwa ama watu kukufatilia wengine kukutishia wengine kujifanya wanakuangalia kimpango, taarifa hizo ni nyingi lakini hivyo sio vitu vya kunitisha wala sitembei na mlinzi na siogopi nitaendelea kufanya kazi ya ukombozi kwa sababu kwanza siwezi kuishi milele, kuna watu hawafanyi harakati za ukombozi lakini wako wanakufa Muhimbili kwa magonjwa kama Malaria”
Kwenye sentensi ya nyongeza naendelea kumkariri Lema akisema “mimi ni bora nikapigwe risasi lakini mchungaji akija kusoma risala aseme marehemu amekufa akipigania haki, kifo kwangu kimeshapoteza kumbukumbu na uoga kwangu umeshapoteza kumbukumbu, siogopi kufa siogopi jela ila naogopa kwenda jela kwa wizi wa kompyuta, Tv au kubaka mwanamke lakini siogopi kwenda jela kwa kupigania haki za watu, wanaoleta vitisho ninawakaribisha.. ni vingi na vingine tunavifanyia utafiti sisi wenyewe tujue chanzo ni nini, hata muundo wa serikali ulivyo dhidi ya wapinzani ni kitisho namba moja, kwamba wewe ni mbunge wa Chadema na unafanya kazi na DC ama na mkuu wa mkoa ambae ni mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilaya”
Kauli nyingine aliyoitoa Lema ni kuhusu kesi yake kwa sasa kwa kusema “sitaki mahakama ya rufaa inipendelee sitaki hata kidogo, ikinipendelea nitalia, nitaogopa nitasikitika nikijua nilifanya makosa ya kuua alafu nikaachiwa huru, niko tayari kurudi kwenye uchaguzi na nitashinda kuliko mbunge yeyote Afrika Mashariki kwa kura za kubeba na Canter ila ninachotaka ni haki itendeke, ila nimepata faraja kwamba anaeiongoza kesi yangu ni jaji mkuu wa Tanzania nikiamini atapitia vipengele vya kisheria vizuri kabisa”
Pamoja na hayo yote, Godbless Lema amesema hajawahi kujuta kuwa nje ya bunge ila anajuta kwa nini Mahakama iliingiliwa na kumfanya ajue matokeo ya kesi siku 14 kabla ambapo namkariri akisema “Halima Mdee alinipa matokeo ya kesi mpaka kifungu kinachokwenda kunibana, Dr Slaa anaingia mahakamani ananiamba mwanangu unakwenda mahakamani lakini hukumu yako itakua hivi, ile kesi hukumu ilivuja kwa hiyo maana yake ilikua ni mpango, ni kitu kimepangwa”
“Kilichoniumiza sio mimi kutokua mbunge, ninaweza kuishi nje ya Ubunge ninaweza kuuza mitumba, ninaweza kuwa dereva wa daladala, ninaweza kucheza soka.. ubunge kwangu sio ajira naweza kuishi maisha mazuri kuliko kuwa mbunge, nimekua mfanyabiashara siku za nyuma sijakwenda Ulaya nikiwa mbunge, nimekwenda ulaya kabla sijawa mbunge nimekwenda karibu nchi 16 na nimefanya biashara lakini nilipopata ubunge nikasema nimepata nafasi ya kutumikia watu”

1 comment:

  1. Godbless Lema, licha ya kuhusishwa na mtandao wa magari, ni mvuta bangi, mdini na tapeli.

    ReplyDelete

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...