Tuesday, September 11, 2012

KISS LA CHRIS BROWN, RIHANNA PIGO LINGINE KWA KARRUECHE


Chris Brown akim-kiss aliyekuwa mpenzi wake Robyn Rihanna Fenty .
New York, Marekani
SIKU chache baada ya mwanadada Karrueche Tran, demu wa Chris Brown kufunguka hadharani kuwa mchizi amemfanya awe msagaji kutokana na mateso ya kimapenzi anayompa, mrembo huyo amelielezea tukio la Chris kum-kiss aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Robyn Rihanna Fenty wakati wa utoaji wa Tuzo za Video Music Award (VMA) kama pigo lingine katika maisha yake.
Akizunguma na gazeti la US Weekly, Karrueche alisema kuwa awali Chriss Brown alimwambia kuwa hawezi kuhudhuria sherehe za utoaji wa tuzo hizo lakini akabadili uamuzi katika dakika za mwisho, mbaya zaidi akaonekana akimpongeza Rihanna baada ya kunyakua tuzo kama yeye kwa kumpiga busu la mdomoni.
“Kitendo kile kinajirudia akilini mwangu na kunifanya nikose raha kupita kiasi. Amenidhalilisha sana, nafananisha tukio hilo na kunipiga mbele za watu au kunivua nguo barabarani. Kamwe sitaweza kumsamehe,” alisema Karrueche kwa masikitiko.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...