Friday, September 14, 2012

DIDA: NDOA IMEVUNJIKA, SIFIKIRII KUOLEWA


Dida Shaibu.

SIKU chache baada ya kutangazwa kuwa ndoa ya Mtangazaji wa Kituo cha Radio Times cha jijini Dar, Dida Shaibu imevunjika, prizenta’ huyo amedai kuwa ishu ya kuolewa tena haipo akili mwake kwa sasa.
Dida alitoa kauli hiyo mapema wiki hii alipokuwa akizungumza na paparazi wetu aliyetaka kujua ukweli kuhusu tetesi kwamba baada ya ndoa yake kuvunjika, mapedeshee kibao wamejitokeza kutaka kumchukua jumla.
“Ni kweli tangu mapedeshee waliposikia nimeachana na mume wangu G, wengi wananipigia simu na kuomba wanioe lakini nimewatolea nje kwa sababu kwa sasa sifikirii kabisa suala la ndoa,” alisema Dida.
Hivi karibuni Dida na mumewe Gervas Mbwiga waliachana, mtangazaji huyo alipoulizwa sababu alisema ni kwa kuwa ndoa yao ilikuwa ya mkataba wa mwaka mmoja licha ya madai kuwepo kuwa, kuna mwanamke mmoja wa mjini ndiyo chanzo.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...