Friday, September 14, 2012

NDIKU ADAIWA KUMRUSHIA DONGO UWOYA


Hamad Ndikumana ‘Kataut’ na Irene Uwoya.

IKIWA imepita miezi kadhaa tangu mcheza kabumbu la kulipwa wa nchini Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ kufungasha virago na kurejea kwao, imedaiwa kamrushia dongo mkewe Irene Uwoya.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, hivi karibuni Ndikumana alitupia maneno yasemayo; “Ningekwambia mengi lakini vyema nikutazame nione mwisho wako”  sentensi ambayo inadaiwa inamlenga Uwoya.
“Huu ni ujumbe kwa Uwoya, inavyoonekana anampenda sana na amekuwa akimuwaza na kuna yale ambayo anayasikia kiasi kwamba anatamani kumwambia abadilike lakini anashindwa ndiyo maana katumia njia hii licha ya kwamba hajamtaja jina,” alisema Mariam mmoja wa walioona ujumbe huo mtandaoni.
Ndoa ya wawili hao inaonekana kuwa kwenye giza nene mpaka sasa huku kila mmoja akiishi kivyake licha ya kwamba hivi karibuni kuna ndugu, jamaa na marafiki wa Uwoya ambao waliapata kuhakikisha wanaihuisha tena.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...