Friday, September 14, 2012

Oprah Talks Exclusively with Usher About Custody Battle - Oprah's Next C...

VIDEO NA MAELEZO KUHUSU INTERVIEW YA USHER RAYMOND NA OPRAH.


Kwa kipindi kirefu watu wamekua wakimtaka usher Raymond aulizwe kuhusu ndoa yake na mkewe wa zamani Tameka, sasa mtangazaji maarufu Oprah ambae huwa anafanya interview na mastaa zinazofichua mambo mengi ambayo huwa hayaongelewi kwengine, amemaliza kufanya interview na Usher Raymond.
Japo Usher amekua akikwepa kuzungumzia ishu zake na mkewe kwenye media amekiri kwamba time hii kwenye show ya Oprah ataongea yote kuhusu uhusiano wake na mkewe wa zamani Tameka, na baada ya hapo hatoongelea tena hiyo ishu... chek sehemu ya hiyo interview hapo chini.

Kwenye hiyo show pia imefahamika kwamba Usher Raymond atazungumza kuhusu kuruhusiwa na mahakama kukaa na watoto wake, kitu ambacho amekigombania mahakamani na mkewe kwa miaka mitatu.
Usher Raymond atazungumza pia kuhusu kitendo cha mama yake mzazi kugoma kuhudhuria harusi ya Usher na Tameka ambapo kwenye line nyingine, atazungumza kuhusu kushindwa kuperform alipokwenda Berlin Ujerumani, ambapo kama unakumbuka alipanda mpaka kwenye stage kabisa lakini muda mfupi tu baada ya kuanza kuimba akasimama ghafla na kuomba radhi kwamba hatoweza kuendelea kuperform kwenye hiyo show ambayo ni kama Serengeti Fiesta.
Baada ya hapo watu walisema Usher ameisha kimuziki, hawezi kurudi tena… sasa kakubali kulizungumzia hilo kwenye interview na Oprah.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...