Monday, September 24, 2012

DIAMOND AENDESHA ZOEZI LA KUSAKA MAMODO WATAKAOSHIRIKI VIDEO YAKE


Diamond Platinumz (katikati) akiongoza jopo la majaji katika zoezi la kusaka mamodo watakaoshiriki video yake.
Mamodo waliofanikiwa kupenya katika mchujo wa awali wakiwa katika pozi.
Baadhi ya washiriki wakionyesha mbwembwe zao wakati wa usaili.
Mama Diamond na dada yake nao walikuwepo katika usaili huo.
MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' jana mchana aliendesha zoezi la kusaka vijana watakaoshiriki katika video yake mpya ambayo bado hajaitaja jina.
Usaili huo wa kwanza wenye lengo la kupata vijana wakali 10 wa kiume na 10 wa kike watakaolamba shavu la kutokelezea katika video mpya ya Diamond ulifanyika katika Ukumbi wa Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wa modo wa kiume, washiriki 18 walipita katika mchujo huo wa kwanza ambapo wataitwa katika fainali itakayotangazwa hivi karibuni. Kwa upande wa modo wa kike, washiriki 16 walifanikiwa kupenya katika awamu hiyo.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...