Monday, September 24, 2012

Shilole Asema "Niliwahi kutafuta Skendo wakati naanza lakini si kukaa uchi"

MSANII ndani ya tasnia ya filamu na muziki, Zena Muhamed ‘Shilole’, ameuambia mtandao wa DarTalk kuwa awali alipoigia kwenye tasnia ya filamu alikuwa anatafuta skendo lakini hata hivyo hakuwahi kujiweka nusu uchi ili ajulikane kwani siku ambayo atafanya hivyo ananaamini hata familia yake na hata mashabiki wanaomkubali watamuona mtu wa ajabu sana.

Msanii huyo alidai kuwa alikuwa na skendo nyingi lakini hakuwahi kuwaonesha watanzania mwili wake kama baadhi ya wasanii wanavyofanya, kwani kitendo hicho endapo angeamua kukifanya basi wazazi wake wangemchukulia kama limbukemi wa maisha ya mjini.

Kauli ya msanii huyo inakuja ili kujisafisha kwani wadau wengi wa tasnia ya filamu kwa sasa hawana hamu nayo, kutokana na vitendo vingi vinavyofanywa na wasanii wake, ambapo vingine vimekuwa vikiwahawaribu hata watoto wadogo ambao hupenda sana kutazama kazi zao.

“Awali wakati naanza filamu nilitamani sana na mimi niwe staa na nikawa natumia njia kibao lakini hakuna hata moja ambayo unaweza kusema imenichafua au kuniacha nikiwa mtupu na watu wakawa wananiona mwili wangu hakuna, lakini nashindwa kuelewa nikwanini mastaa wazima wanatumia miili yao kuongeza umaarufu wakati wanajitia doa tu,” alisema.

Hata hivyo msanii huyo aliongeza kuwa anaamini pia kwa kaisi kikubwa muziki nao umempa umaarufu sana, kwani amejizolea mashabiki wengi ndani na nje ya nchi, hasa wale wanaopenda aina

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...