Friday, September 7, 2012

BBAMED AHUDUMIA WATEJA HUKU AIWA NA MTOTO MGONGONI

Na Mwandishi Wetu
KWELI wanaume ni noma! Msichana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Veronica, amelazimika kufanya kazi ya kuhudumia wateja baa ‘baamedi’ huku akiwa na mtoto wa kumzaa mgongoni.
Veronica alinaswa juzikati saa sita usiku katika Baa ya Uswaa iliyopo maeneo ya Mji Mpya, mkoani hapa.
Alikuwa amembeba mwanaye huyo kwa kutumia kitenge huku akisema asitafsiriwe kama amekusudia kufungua vizibo na mtoto mwenye mwaka mmoja mgongoni bali mwanaume aliyempachika mimba aliikataa na kuingia mitini.
Baamedi huyo alisema mwanaume huyo aliikataa mimba yake kwa madai kwamba, mkewe akijua ndoa yake haitakuwa hai tena jambo ambalo mwanaume huyo hakulitaka litokee.
“Nilikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mmoja jina namhifadhi kwa kuwa ni mume wa mtu, ni dereva wa treni. Kipindi chote cha uhusiano hajawahi kunitamkia kuwa ana mke, nilipomueleza kwamba nina ujauzito wake akaniambia niutoe kwa kuwa yeye ni mume wa mtu.
“Nilikataa kuutoa mpaka nikajifungua, tena namshukuru Mungu maana nilijifungua salama kabisa, kutokana na ugumu wa maisha huku nina mtoto ndiyo ikabidi nitafute kazi hii ya baa kwa lengo la kupata fedha za kujikimu na maisha,” alisema Vero.
Hata hivyo, baadhi ya wateja kwenye baa hiyo walimshauri kwenda mbele zaidi, kama Ustawi wa Jamii ili mwanaume huyo aitwe na kuwekewa amri ya kutoa fedha za matumizi kila siku kuliko kuendelea kuuza baa na mtoto kwani mwisho wake ni kumbemenda.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...