Friday, September 7, 2012

ALIYEVUNJA NDOA YA DIDA NI HUYU


Na Mwandishi Wetu
MWANAMKE anayedaiwa kusababisha ndoa ya Mtangazaji wa Redio ya Times FM ya jijini Dar es Salaam, Khadija Shaibu ‘Dida’ na mumewe Gervas Mbwiga ‘G’  kuvunjika ametajwa kuwa ni Tecla Benedict, Amani limejazwa data za kutosha.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mwanamke huyo ametajwa kuwa ni chipukizi wa Bongo Fleva akiwa mwanafunzi wa chuo kimoja kilichopo jijini Dar.
Kikitoa undani wa kisa cha ndoa hiyo kuvunjika, chanzo chetu hicho kimesema kuwa, Tecla alituma ujumbe mfupi wa maneno (sms) kwa mume wa mtangazaji huyo na kunaswa na Dida.
“Dida alianza kuchati na Tecla bila ya mwanamke huyo kujua kama alikuwa akichati na mwanamke mwenzake na kuweka bayana kwamba alikuwa mjamzito kitendo kilichomchefua Dida,” kiliendelea kusema chanzo hicho.
Kikasema kuwa, kesho yake Dida alimpigia simu Tecla na kumwagia matusi na kumpa vitisho huku akimwambia kuwa ajiandae kuachiwa mume.
Baada ya kuona hivyo, Tecla alilazimika kubadili namba ya simu kwa kuhofia kuendelea kuandamwa na Dida.
Mwandishi wetu baada ya kupata habari hizi, alimpigia simu Tecla ambaye alikubali kuwa na uhusiano na mume wa Dida, G huku akidai kuwa hakuwa akifahamu kama mwanaume huyo ni mume wa mtangazaji huyo.
 “Siyo kosa langu kwani hata siku moja sikuwahi kumuona na pete, nilipomhitaji wakati wote alikuwa karibu na mimi, wala hakuwahi kuniambia kama ameoa,” alisema Tecla.
Mwandishi wetu pia, alimvutia waya G na kumuuliza kama ni kweli  Tecla ndiye chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yake na Dida, hata hivyo G hakutoa ushirikiano wa kutosha.
“Naomba unipigie baadaye kwani muda huu utanikosesha umakini, niko kwenye kikao, tutaongea baadaye,” alisema G na kukata simu.
Dida alipotafutwa  alisema kuwa, hakuwa tayari kuzungumzia habari hizo kwa kuwa ameshaachana na mwanaume huyo.
“Tafadhali ndugu sina muda wa kuzungumza masuala hayo, niko serious (makini) na mambo yangu ya msingi…” alisema.
Ndoa ya Dida na G ilivunjika hivi karibuni baada ya kutimiza mwaka mmoja, awali ilidaiwa kuwa ilikuwa ni ndoa ya mkataba wa mwaka mmoja na ilivunjika kutokana na tofauti za kidini kati ya wawili hao.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...