Saturday, September 8, 2012

ISABELLA anaswa akifua rundo la ‘makufuli’MISS Ruvuma 2005 ambaye pia alipata ‘leseni’ ya kushiriki Miss Tanzania mwaka huo na asiyekaukiwa na skendo, Isabella Mpanda juzikati alinaswa akifua nguo kibao za ndani.
Ishu ya usafi huo ilikuwa Septemba 5, 2012 nyumbani kwa staa huyo anayewakilisha kundi la Scorpion Girls, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam tena uani.
Mapaparazi wetu walitia timu kwenye makazi yake hayo kwa lengo la kumuuliza tetesi zilizoenea kwamba, yeye na mchumba wa mwigizaji staa, Jack Wolper, Dallas ni wapenzi ambapo alikanusha  vikali madai hayo.
Aidha, alipoulizwa ni kwanini anaacha nguo za ndani mpaka zinakuwa nyingi ndipo afue na ana muda gani hajafua viwalo hivyo, Isabella alifunguka hivi:
“Aaaah! Kwa kweli ni muda mrefu sana, unajua nini? Huwa navaa mpaka ichafuke nachukua mpya, ndiyo maana zikawa rundo namna hii.”
Paparazi: Huwa unavaa hadi ichafuke unachukua mpya?
Isabella: Ndiyo.
Paparazi: Ina maana unaweza kuvaa kufuli moja kwa siku tatu?
Isabella: (kicheko), siyo hivyo jamani! We unadhani mwanamke anaweza kuvaa nguo ya ndani kwa siku zaidi ya moja, labda wanaume.
Isabella alisema ana tabia ya kununua nguo za ndani nyingi, kwa hiyo kila siku anavuta moja mpya na kuibandika mwilini ndiyo maana anajikuta akiwa na mzigo wa kutosha wakati wa kufua.
Hata hivyo, licha ya kumkuta akifanya usafi wa nguo zake hizo, mrembo huyo alikuwa na glasi mkononi ikiwa na bia ambapo alidai ndiyo maisha yake ya kila siku.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...