Tuesday, September 4, 2012

BABU ALIYEFUMANIWA NA MPANGAJI WAKE ASUSIWA MKE


SIKU chache baada ya gazeti ndugu na hili, Risasi Jumamosi kuripoti juu ya fumanizi la babu mwenye umri wa miaka 70, Rafael Mitasio aliyenaswa gesti akiwa na mke wa mpangaji wake, taarifa tulizozinasa zinadai kuwa mzee huyo amesusiwa mwanamke huyo.
Chanzo chetu cha habari kimedai kuwa, mara baada ya habari hiyo kutoka gazetini, mume wa mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la baba Tausi aliumia sana hivyo akampa kisogo kitendo kilichomfanya mgoni huyo atangaze kumuoa.
“Ile habari ilipotoka kwa kweli mume wa yule mwanamke aliumia sana, akaamua heri huyo mzee amchukue kabisa kama ameona anaweza kumtunza kuliko yeye.
“Cha kushangaza yule mzee naye eti anadai wala habari hiyo haijamuumiza na anasema atamuoa kabisa mwanamke huyo ili kuwakata vilimilimi wabaya wake,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Kufutia taarifa hizo, Uwazi lilimtafuta baba Tausi lakini hakuweza kupatikana mara moja. Mzee Rafael alipotafutwa kuzungumzia kama kweli ana mpango wa ‘kumchukua jumla’ mwanamke aliyenaswa naye wakivunja amri ya sita, alizungukazunguka sana lakini mwisho akasema:
‘’Si mmeshaandika kuwa nimefumaniwa, haya kaandikeni tena kuwa nataka kumuoa kabisa ili mfurahi.”
Mzee Rafael aliripotiwa kufumaniwa hivi karibuni kwenye gesti ya Sekei iliyopo mjini hapa akiwa na mke wa mpangaji wake.
Tukio hilo liligeuka kuwa gumzo katika maeneo mengi ya mji huku wengi wakishangazwa na kitendo cha mzee huyo kumshawishi mke wa mpangaji wake mpaka wakanaswa wakiwa watupu gesti.
Hata hivyo, fumanizi hilo lilizua kizaazaa cha aina yake hadi likafikishwa polisi.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...