Tuesday, September 4, 2012

NYUMBA YA LULU YADODA

Elizabeth Michael ‘Lulu’.

NYUMBA ya msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ (pichani) iliyopo maeneo ya Golani, Kata ya Saranga, wilayani Kinondoni jijini Dar sasa imedoda kufuatia mwanadada huyo kuwa gerezani akihusishwa na kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba.
Chanzo chetu cha habari ambacho kinaishi maeneo hayo kililiambia Uwazi kuwa, kabla ya Lulu kukutwa na matatizo hayo, ujenzi wa nyumba hiyo yenye vyumba sita ulikuwa ukienda kwa haraka lakini sasa hivi umesimama.
“Kimsingi ile nyumba ya Lulu kule Golani imedoda, ujenzi unaenda kwa kusuasua sana tofauti na kipindi cha nyuma,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake na kuongeza:
“Mwenyewe alikuwa akisema anataka kufanya haraka ili ahamie mwezi uliopita, ndoto zake zimeyeyuka, sasa imefikia kwenye linta na uendelezaji wake si wa kivile.”
Baada ya kupata habari hizo, Uwazi lilifika maeneo ilipo nyumba hiyo na kufanikiwa kuiona ikiwa katika mazingira ya kudoda na lilipozungumza na mjumbe wa Tawi la Saranga, Bi. Cristina Emmanuel alisema:
“Nyumba hii baada ya Lulu kufikwa na matatizo, mama yake ndiye aliyekuwa akija kuiendeleza lakini katika siku za hivi karibuni, ujenzi umesimama.”

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...