Friday, September 21, 2012

AUNTY LULU ATIMULIWA NA MWENYE NYUMBA


Lulu Mathias Semagongo 'Aunty Lulu'.
Na Gladness Mallya
MWANADADA asiyeishiwa na matukio Bongo, Lulu Mathias Semagongo 'Aunty Lulu' amefukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa anaishi Kinondoni jijini Dar es Salaam kutokana na mmoja wa wanaume aliokuwa akiishi nao anayedaiwa kuwa 'si riziki' kufumaniwa akifanuya uchafu chooni.
Akizungumza na Ijumaa, mmoja wa majirani wa Aunty Lulu ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini alisema mwanadada huyo pamoja na wanaume aliokuwa akiishi nao walifukuzwa wiki iliyopita na mwenye nyumba baada ya kubaini kuwa, wanatumia chumba chao kufanya ufuska.
“Yaani sijui kwa nini Aunty Lulu alikuwa anawang’ang’ania wale mashoga, yaani walikuwa wanatusumbua kweli mpaka mwenye nyumba kaamua kuwafukuza, kitendo cha kufumwa chooni siyo cha mara ya kwanza, hii ni mara ya pili,” alisema jirani huyo.
Baada ya kuzinyaka ‘nyuuzi’ hizo paparazi wetu alimtafuta Aunty Lulu ambapo alikiri kufukuzwa ndani ya nyumba hiyo kutokana na tabia za wanaume hao ambao walikuwa wamepinda ile mbaya.
“Ni kweli, wale watoto wameniharibia sana na sasa naishi kwetu huko Mbezi wakati natafuta chumba kingine,” alisema Aunty Lulu.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...