Friday, September 21, 2012

NYUMBA YA AFANDE SELE YAZINGIRWA, MTAA WAFUNGA, KISA WEMA


Selemani Msindi ‘Afande Sele’ akiwa na staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.

NYUMBA ya mwanamuziki  Selemani Msindi ‘Afande Sele’ iliyopo Misufini mkoani hapa, mwishoni mwa wiki iliyopita ilizingirwa na watu kibao waliotaka kumuona na ikiwezekana kumgusa staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Wema alifika nyumbani hapo saa 7 mchana kwa lengo la kumjulia hali mke wa Afande Sele, Asha Msindi ‘Mama Tunda’ ambaye hivi karibuni alijifungua mtoto wa kike aitwaye Asantesana.
Staa huyo akiwa ndani ya nyumba hiyo, mtaa ulijaa watu wa maeneo hayo kwa lengo la kumshuhudia mwanadada huyo ambapo baadhi walifanikiwa kumuona na kufarijiki kwani walizoea kumuona kwenye TV tu.
Muda wote Wema akiwa nyumbani hapo, mama Tunda alionekana mwenye furaha na kumshukuru msanii huyo kwa kufika kwake kumtembelea.
Aidha, wakazi wa eneo hilo walimfagilia Wema kwa kuwa na moyo wa upendo na kumtaka siku nyingine awatembelea na awape muda wa kutosha kuwa naye.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...