BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Friday, September 7, 2012

PASTOR MYAMBA: KANUMBA ALINITONYA KUHUSU FREEMANSON



MSANII ‘first class’ katika kiwanda cha filamu za Kibongo, Emmanuel Myamba ameibuka na kudai kuwa marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake aliwahi kumtonya kuhusiana na masuala ya Freemanson.
Akizungumza na Ijumaa juzikati, Pastor Myamba alisema siku hiyo Kanumba alitumia muda wake mwingi kuzungumzia masuala ya Freemanson, jambo ambalo lilimfanya abaki na maswali mengi kichwani.
 “Nakumbuka sana Kanumba aliwahi kuzungumzia sana masuala ya Freemanson, alikuwa ananionyesha kwenye intaneti jinsi Freemanson wanavyofanya kazi zao lakini sikufahamu kama alikuwa na mkakati wa kujiunga nao au vipi,” alisema Myamba ambaye hivi karibuni alizindua chuo chake cha masuala ya filamu chini ya Kampuni yake ya Bornagain Film Productions.
Kanumba na Pastor Myamba walikuwa marafiki wa karibu sana na baada ya Kanumba kufariki, taarifa za kwamba alikuwa Freemasons zilizagaa sana kiasi cha kuwashangaza wengi.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...