Serikali ya Kenya imetishia
kuwafuta kazi walimu ambao wamekuwa wakigoma kwa wiki tatu sasa na
kuwaajiri walimu wapya waliofuzu pamoja na walimu waliostaafu ikiwa
hawatarejea kazini hii leo.
Makataa hii inakuja baada ya vyama vya walimu kukataa pendekezo la nyongeza ya mishahara ambayo wangelipwa kwa awamu tatu.
Walimu hao wanataka nyongeza ya
aslimia miatatu ya mishahara, pesa ambazo serikali inasema haiwezi
kumudu kwa sasa kwa sababu ya hali mbaya ya kiuchumi.
Mgomo wa walimu umesababisha kufungwa kwa shule
za umma kwa zaidi ya wiki tatu sasa wakati wanafunzi wakijiandaa kwa
mitihani ya kitaifa.
Huenda serikali ikalazimika kuakhirisha mitihani
hiyo ya kidato cha nne na darasa la nane inayotarajiwa kuanza katika
muda wa wiki chache zijazo.
Madaktari wa hospitali za umma pia wanafanya
mgomo wa kitaifa huku hospitali hizo zikiwahudumia tu wagonjwa walio
katika hali ya dharura.
No comments:
Post a Comment