Wafanyakazi katika mgodi mmoja
wa dhahabu nchini Afrika Kusini,AngloGold wameanza mgomo mpya ambao ni
wa hivi karibuni kukumba sekta ya madini nchini humo.
Mgodi wa Kopanang anawaajiri wafanyakazi elfu
tano na wanagoma wakitaka mishahara yao kuongezwa zaidi ya mara mbili
hadi randi 12,500 au dola 1,513.
Mgomo huu unakuja siku moja baada ya
wachimba migodi wa mgodi wa Marikana kusitisha mgomo wao baada ya
kuafikia makubaliano kuhusu nyongeza ya mishahara.
Uchunguzi kuhusu vifo vya zaidi ya wachimba migodi 40 unatarajiwa kuanza tarehe moja mwezi ujao.
Waziri wa sheria, Jeff Radebe alisema kuwa
familia za watu 34 waliouawa na polisi,watashauriwa kuhudhuria kwenye
uchunguzi huo, na kwamba utachukua miezi minne kukamilika.
Afrika Kusini ni mojawapao ya nchi zinazozalisha madini kwa wingi sana duniani.
Zaidi ya asilimia themanini ya madini ya dunia ya Plattinum hutoka nchini humo.
Takriban wafanyakazi 15,000 wanaoajiriwa na kampuni ya dhahabu ya AngloGold wanagoma.
Inakisiwa asilimia saba ya uzalishaji wa dhahabu
nchini Afrika Kusini uliathirika kutokana na migomo mingi ambayo
imekumba nchi hiyo.
Mgomo huu wa hivi karibuni ulianza usiku wa kuamkia leo katika mgodi wa Kopanang Magharibi mwa mji wa Johannesburg.
Inaaminika kuwa mgodi huo huzalisha asilimia ishirini ya dhahabu inayotoka Afrika Kusini.
Matakwa ya wachimba migodi hawa ni sawa ya wale
wa mgodi wa Marikana ambao baadaye walikubali nyongeza ndogo ya
mishahara kuliko walivyokuwa wanadai.
No comments:
Post a Comment