Wawili hao walinaswa wakijiachia kwa raha zao huku wakionesha waziwazi kukolezana kimalavidavi ambapo baada ya kuwafotoa picha kadhaa, mwandishi wetu alitaka kufahamu ukweli wa uhusiano wao ambapo wote walikiri kuwa wanatoka kimapenzi.
“Kweli natoka na Shilole kimapenzi lakini naomba usiandike gazetini maana utaniharibia mambo yangu mengi kwa mabosi wangu,” alisema Ombeni huku Shilole naye akithibitisha suala hilo na kueleza kuwa walisafiri pamoja kutoka Dar, naye akaomba ishu hiyo isichorwe gazetini. Baada ya kujiachia kwa sana, wawili hao waliondoka na kwenda kulala pamoja.
No comments:
Post a Comment