Tumeona takwimu zilizotolewa siku za karibuni
kuwa moja ya mitandao jamii yaani Facebook wamefikisha watumiaji zaidi
ya milioni mia tisa, hiki ni kiwango kikubwa mno,sasa tunaweza kujiuliza
je ni kwanini watu wengi wamekuwa wakikimbilia huko,sababu kubwa ni
kuwa kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza. Lakini hizi takwimu kwa
upande mwingine zinaweza kutupa changamoto mbalimbali za kuweza
kuangalia mengi yake,kwani kila siku zinavyozidi kwenda mbele ndio wana
jamii wetu wengi wamekuwa wakijiunga humo,hivyo sisi kama wadau wa ICT
management ni kazi yetu kuangalia kwa undani hii mitandao jamii ili
tuweke wazi kila kitu ili isije kuathiri jamii yetu ya Kitanzania na
Afrika mashariki kwa ujumla.
Kitu kimoja kinachoniumiza kichwa ni kuwa,
kwenye mitandao hii,mtu unaweka mambo yako mengi mno wazi,ingawa kuna
uwezo wa kuficha ila kwa kufanya hivyo malengo ya matumizi yatakuwa
hayajapatikanika,hivyo uamuzi unabaki kwako,weka wazi ili watu waone au
usijiunge,kwani katikati yake hakuleti ufanisi.Hofu yangu ni kuwa,wengi
wetu tumekuwa tukijaza mambo kibao kwenye hii mitandao jamii,itakuja
siku mtu atajikana mwenyewe au kubadilisha jina kwakuwa jina lake
limechafuliwa sana kwenye mitandao jamii.Binafsi kuja kwa mitandao jamii
kumenifundisha jambo kubwa moja,siri binafsi,nini natakiwa kuwapa watu
waone na nini kitaendelea kuwa changu binafsi na watuu wa karibu tu.
Faida zinazopatikani na hii mitandao jamii ni kubwa mno,binafsi nimeweza kukutana na rafiki yangu tuliyekuwa naye tangu vidudu na shule ya msingi halafu kupoteana,kwa kutumia Facebook nimeweza kuonana naye tena tukiwa mbali mno,hii inaonesha umuhimu wa hii mitandao jamii.Mitandao jamii imeleta mapinduzi makubwa mno kwenye tovuti,mfano ni Twitter,unaweza kupata habari iliyotokea dakika chache moja kwa moja,kwa nchi zilizoendelea wamekuwa wakitumia Facebook ama Twitter kama njia mojawapo na thabiti ya kampeni,hivyo ukweli unabaki palepale bado tunaihitaji,ila kwa tahadhari.
Tatizo kubwa la hii mitandao jamii ni kuwa,kwa sekunde moja unaweza kuharibu jina na hadhi yako moja kwa moja,baya zaidi ni kuwa kitu ukishakiweka kwenye mitandao ni ngumu kukifuta tena,kwani hata kama utaondoa kuna wajanja au website zinazohifadhi mafaili hayo,pia kuna watu ambao wapo haraka,ndani ya sekunde akishaona kitu chenye muelekeo hukiifadhi kwenye kompyuta yake kwa amatumizi ya baadae. Ni wangapi wamevunja ndoa zao kwakuwa ameona picha ya mchumba yake yupo na msichana au mvulana mwingine.Binafsi kipindi nikiwa webmaster wa website ya wanafunzi wa kigeni hapa Wuhan,China,pia tulikuwa na ukurasa wa facebook(facebook page),nilikuwa napokea malalamiko kila kukicha watu wakilalamika kufuta picha kadhaa zilizowekwa na members zikiwaonesha wakiwa kwenye majumba ya starehe kwakuwa nyumbani wakijua ni mwisho wa shule,Niliwahi kujiwa na mdada wa kisomali huku akilia kwakuwa kama ile picha ikionekana kwao basi ana adhabu kali mno.Kumbuka jamabo unaloliona ni la kawaida leo linaweza kuwa ni kizingiti kwako miaka kumi ijayo kwani watu huifadhi kumbukumbu hadi pale itakapokuwa na umuhimu.
Tukiachana na hayo hebu tuangalie mambo mengine yaliyo nyuma ya panzia la hii mitandao jamii.

Kusaka ajira
Siku hizi kuna baadhi ya wajiri hutaka kupata kumbukumbu za mhusika
kwenye facebook ama Twitter kwa siku za karibuni,kwani wao wanatambua au
kuamini kuwa huko wanaweza kukujua wewe halisi,unaweza kusema njia ni
rahisi tu,nitafuta,ila sio kila kitu kinafutika pia sio rahisi kwako
kujua kama watahitaji hivyo unajikuta unapambana nayo siku ya siku..
Kwa kutumia mitandao hii unaweza kumjua mtu katika hali halisi na sio
majificho ndani ya interview.Nimewahi kuongea na muajiri mmoja kuhusu
hili,yeye alisema kuwa jambo muhimu katika kuajiri ni kupata mtu asilia
na anayeweza kufanya kazi kwa timu na mahali pa kuzipata hizi ni kwenye
mitandao jamii.
Kupoteza ajira
Wangapi wamekuwa wakipoteza kazi kutokana na ujumbe wao walioweka
kwente facebook au Twitter,nimewahi kusoma makala moja,jamaa alikuwa na
matatizo na Bosi wake,yeye akaamua kuhamishia bifu kwenye
facebook,akaweka ujumbe mzito pale,watu bila kuchelewa wakaanza
kumalizia hasira zao za zamani na yule bosi,basi mpaka bosi anapelekewa
taarifa na wapambe wake tayari alikuwa kashavulika nguo,unategemea nini
kitafuata? Sio hilo tu,wewe uunaweza kuwa na lengo zuri labda la kutaka
kuomba ushauri kwa marafiki zako lakini kila mtu ana uwezo wake wa
kupambanua mambo na hao ndio watakaokuweka matatani.
Kutilia mkazo hili,kipindi kimoja nilikuwa manager kwenye sehemu
fulani,tukaandaa sherehe,baada ya sherehe kuna member wetu wa ndani
alituma picha kwenye facebook kumuonesha mfanyakazi mwingine aliyekuja
kwenye sherehe kama anaenda msibani na akaacha kibwagizo,msiba au
sherehe?,watu waliacha maoni ya kudharirisha.Ilinibidi nifanye maamuzi
magumu pale ya kumuondoa mhusika kwenye kile kitengo.
Marafiki wanaokuzunguka
Sio siri ukweli ni kuwa maranyingi marafiki zako huweza kutoa picha
yako kamili,hapa ninamaanisha watu wanaweza kukujua au kukuthaminisha
kutokana na kundi la marafiki zako,kipindi nikiwa mtoto nilikuwa napewa
mafundisho kuwa ukitembea na mwizi nawe utakuwa mwizi hivyo nilitakiwa
kuwa na marafiki wanaofanya vizuri darasani,kuna methali kadhaa za
kiswahili zinazotilia mkazo hili(Ukitembea na muuza….[imenitoka
kidogo]). Sasa siku hizi kuna baadhi ya watu hupenda kukuthaminisha
kutokana na kundi la marafiki ulionao kwenye mitandao
jamii,inawezekanika wewe mwenyewe hujui hili ila lipo.Baadhi ya mabenki
ya nchi fulani fulani wamekuwa wakitumia hii kuangalia kipato cha
marafiki zako na wewe binafsi kwa kuangalia picha na maisha yako
halisi,unatumiaje pesa zako,unamiliki nini nk ili kupitisha mikopo yote
haya yanaweza kupatikanika ndani ya mitandao jamii.
Mahusiano
Inawezekana kuwa mpenzi au mchumba wako ni mmoja wa marafiki zako
kwenye facebook au twitter,na ataendelea kuwa rafiki,kumbuka wengi wetu
tumekuwa tukiona wapenzi wakitoa maoni mbalimbali juu yao yakiambatana
na ahadi kemkem,watu wanaangalia na kuyahifadhi,nani anajua nini
kitatokea kesho? unaweza kujikuta unajiingiza kwenye msongo wa
mawazo.Kuna rafiki yangu aliwahi kuandika maoni ya kwenye picha yake ya
harusi kwenye facebook kuwa “Sisi tumechaguliwa na mungu,siku
nitapoachana nawe basi kichwa changu kata”,ujumbe kama huu unaweza
kukusababishia matatizo baadae,oho,watu watataka kuja kukichukua kichwa
chao.Kwani mapenzi ni mapenzi,nani anajua nini kitatokea kesho?
Mahakamani
Sina uhakika kwa nyumbani,ila kwa nchi za wenzetu mawakili au
mahakimu hutumia sana kumbukumbu za mitandao jamii kupata ukweli wa
jambo fulani,ujumbe ulioandika miaka mitatu iliyopita kuhusu kumchukia
kwako bwana Kilongwe inaweza kusaidia mawakili kukupata kiundani,mfano
mzuri tu kuna kipindi nilikuwa nafanya utafiti wa jamaa waliokuwa
wanatuma e mail za kashfa kwenye yahoo group letu.Baada ya kupitia njia
fulani fulani za Forensic nikaja mwisho kutumia mitandao jamii kumbaini
ni nani aliyekuwa anafanya maupuuzi,tangu hapo alikuwa mpole kwani
nilimtumia kila kitu kuonesha uhusiano wake.
Kuna usemi wa kingereza unasema “an elephant never forgets”.Sasa
kumbuka kuwa Internet nayo haisahau kwenye internet kuna idadi kubwa ya
hazina ya kumbukumbu ambayo inaweza kupatikanika ndani ya sekunde
,ahsante mitandao kama Google inayotuwezesha kupata mambo matamu kama
haya.
Binafsi sitaki kuwatisha au kuwafanya watu wanze kutumia majina
bandia kama kwenye sehemu fulanifulani za udaku,ila napenda kutilia
mkazo, kuwa makini juu ya kitu gani unatuma na kitu gani kitaendelea
kuwa kwenye hazina yako,tafakari kwa undani na sio kujitumia kwani ipo
siku unaweza kujijutia na kuichukia hii mitandao jamii. Nimeongelea
machache tu ili mada isiwaboe.
No comments:
Post a Comment