Katika dunia ya leo internet ni kitu muhimu
kwa maisha ya kila siku,sio tu kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kazi
bali hata kwa kuongeza mahusiano kati ya wanajamii. Vilevile makampuni
mengi yamekuwa yakitumia internet kama sehemu muhimu ya kufanyia
biashara.Wengi wetu tumekuwa tukitajataja majina au anuani za tovuti
nyingi kama afroit,google,baidu nk kwa urahisi,wapo ambao hatufahau
kwanini baidu na si google,kwanini haya majina ni ya kipekee na
hayafanani.Hayo yote ndio yanaitwa domain name. Leo,mdau atafafanua
domain names kwa undani na kukupa mdidi tosha,tutaweza kujua ni nini
Domain name,kwanini tunatumia,faida za kutumia na mambo ya kuzingatia
kabla ya kuchagua Domain name. Domain name ni nini?
Kila kitu kilichopo kwenye internet
kina asili au chanzo chake kinapotoka,ambayo hutambuliwa kwa kutumia
muunganiko wa kanuni na sheria nyingi,kwa lugha za kiufundi hujulikana
kama Uniform Resource Locator (URL).Domain name ni sehemu ya
hii anuani(URL) ambayo hupewa kila tovuti au seva iliyopo kwenye
internet ili kujitofautisha au kujitambulisha kwa nyingine.
Mfano mzuri wa Domain name ni “www.afroit.com”.Inasomwa
toka kushoto kuelekea kulia,www inasimama badala ya world wide
web,halafu afroit ni jina la mmiliki,vilevile kuna wakati unaweza
kukutana na Domain name za daraja
la pili,mfano blog.afroit.com hapa “blog” ni domain ya daraja la pili ambayo imesajiliwa na kampuni au tovuti ya AfroIT.
Kulia kabisa utakuta kuna “com” ambayo tunaiita domain level daraja
la kwanza,mara nyingi huwakilisha dhumuni la tovuti au kampuni au mdau
anayemiliki domain.Tukiangalia kwa undani utaona Domain za daraja la
pili ni kama motto wa mmiliki wa Domain name.Hizi domain za daraja la
kwanza domain namezimegawanyika kutegemeana na dhumuni au malengo ya
kampuni,tuangalie michanganuo mbalimbali ya hizi domain za daraja la
kwanza.
.com Humaanisha biashara au huduma iliyokaa
kibiashara(commercial),hivyo kama unataka kusajili tovuti ambayo
itatumika kwa matumizi ya kibiashara basi .com ndio chagua
malidhawa.Ingawawamiliki wa tovuti nyingi zimekuwa zikikimbilia .com
kutokana na umaarufu na mazoea ya .com kulinganisha na domain nyingine
za daraja la juu.
.gov/go Kwa ajili ya matumizi ya kiserikali,tovuti
yoyote ambayo haina uhusiano au si ya serikali hairuhusiwi kutumia
domain name zenye .gov,mfano wa website zenye .go ni kama http://www.tanzania.go.tz.
.edu/.ac Kwa ajili ya matumizi ya kielimu,mfano mashule,vyuo,nk ,www.udsm.ac.tz auwww.znufe.edu.cn ni baadhi ya mifano dhahiri.
.org Kwa makampuni au mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo hutoa huduma kwa jamii(NGO),kwa mfano http://plan-international.org/
vilevile hutumiwa na makampuni au taasisi ambazo mara nyingi huwa
haziwezi kuingia kwenye makundi mengine ya domain daraja la kwanza
.net Kwa wanaotoa huduma za internet,kwa mfano http://www.telecomcareers.net/
Na
nyingine nyingi ambazo hazitumiki kwa wingi,hivyo ni muhimu kuzingatia
dhumuni na malengo ya kampuni au taasisi kabla ya kusajili Domain name.
Ili kuweza kurahisisha utambulishi,Domain name pia huweza kusajiliwa
kutegemea na mgawanyo wa kijiografia.Kwa mfano hapa Tanzania tunatumia
.tz ikimaanisha Tanzania,kenya wanatumia .ke wakani China wanatumia .cn
ikimaanisha China.
Kampuni iliyopo Tanzania inaweza kusajili Domain ya kwanza kama .com vilevile inaweza kusajili kama.co.tz. Kwakuwa Domain za kwanza(top level Domains)hushughulikiwa na InterNic ambayo huwa haiangalii mgawanyiko wa kijiografia, hivyo kila domain ya kwanza hutambulika kiupekee,mfano kama Domain name ya afroit.com tayari imeshasajiliwa,basi Domain name hiyo haiwezi kusajiliwa na mtu mwingine yeyote ili kuondoa muingiliano wa domain.Hii inarahisisha kazi kwa makampuni yanayofanya biasha za kimataifa ambayo hutumia Domain moja dunia nzima.
Kampuni iliyopo Tanzania inaweza kusajili Domain ya kwanza kama .com vilevile inaweza kusajili kama.co.tz. Kwakuwa Domain za kwanza(top level Domains)hushughulikiwa na InterNic ambayo huwa haiangalii mgawanyiko wa kijiografia, hivyo kila domain ya kwanza hutambulika kiupekee,mfano kama Domain name ya afroit.com tayari imeshasajiliwa,basi Domain name hiyo haiwezi kusajiliwa na mtu mwingine yeyote ili kuondoa muingiliano wa domain.Hii inarahisisha kazi kwa makampuni yanayofanya biasha za kimataifa ambayo hutumia Domain moja dunia nzima.
Jinsi Domain name inavyofanya kazi
Dhumuni kubwa la domain name ni kurahisisha utambuzi wa tovuti.Yao
husimama badala ya anuani ya IP, kwa mfano IP address yenye anuani
kama “193.45.0.9″ huweza kuwakilishwa na domain name ya
tanzmed.com..Hivyo basi badala ya mtumiaji kuandika namba ambazo ni
ngumu kukumbuka basi anaandika Domain name,baada ya hapo kuna kompyuta
za kiwango cha juu(DNS Server -Domain Name System Server) hufanya kazi
za kutafsiri domain kwenda IP address halafu kuunganisha maombi kwenda
kwa kompyuta husika,kama fundi mitambo wa TTCL anavyounganisha simu
vile.
Faida kubwa ya kutumia domain name ni kuwa,haiitaji kubadilika hata
kama anuani ya IP inayowakilisha kompyuta au seva itabadilika,kumbuka
kuna sababu nyingi zinawweza kukupelekea kuhitaji kubadilisha anuani ya
IP,ikiwemo kuhama toka kwa mtoa huduma mmoja kwenda kwa mwingine. sasa
basi, hata kama itatokea mbadiliko wa anuani yaIP,bado watumiaji wako
basiwataendelea kukupata,kwani wengi wao hata hawatojua kama anuani yako
ya IP imebadilika,huo ndio msaada ya domain name.katika mabadiliko kama
haya,kinachofanyika ni kubadilisha muunganisho wa Domain name na IP ili
kuunganisha kwenye IP mpya. Ni ukweli usiofichika kuwa Domain name
inaleta mdidi kulinganisha na uchominambavu ambayo ipu kwenye IP
address.
Jinsi ya kuchagua Domain name
Kama tulivyoona,Domain name ndio utambulishi wa tovuti yako kwenye
Internet,hivyo uchaguzi wa Domain name ni lazima ufanyike kwa kuzingatia
mambo mengi,ni ngumu kuyafafanua yote hapa ila nitakueleza kwa uchache
tu kama ifuatavyo
Domain name yako iwe website yako
Domain name ni lazima iendane na website yako,hivyo kuleta maana
tosha ya website,kwa mfano mtu akisikia AfroIT kichwani kunakuja picha
ya mambo mawili Africa na IT,hivyo haimpi tabu kuyakinisha shughuli au
lengo la tovuti
Rahisisha domain yako
Kwa mfano wewe ni muuza magari,sasa unafikiria website yako kuiita
magari.com au kutumia brand mojawapo ya magari yako mfano mikweche.com
ambapo mikweche ni brand mojawapo,mara nyingidomain ya pili inaleta
maana zaidi kwani inakuwa ya kipekee zaidi.
Tumia Domain fupi
Lengo la domain nikurahisisha kazi au kumuwezesha mtumiaji kukumbuka
kwa urahisi,hivyo kutumia domain ndefu kunaweza kuwaletea watumiaji
matatizo ya kukumbuka,ingawa kuna majadiliano kuhusu matumizi ya domain
defu au fupi,ila binafsi bado nashauri matumizi ya domain fupi,mfano
domain kama ibm.com ni rahisi kukumbukika ukilinganisha na
Microsoft.com,leo hii website nyingi za china wanapendelea kutumia
namba,mfano 126.com m18.com nk ambapo ni rahisi zaidi kukumbukika kwao.
.Com,org,net.etc?
Kama umenisoma hapo juu nimeongelea umuhimu wa kutumia domain
kulingana na dhumuni la website,hii ni kweli ila kuna wakati inaweza
kukuletea matatizo fulani,ni wangapi wamekuwa na mazoea ya kutumia .net?
mfano ingekuwia vigumu vipi kama ungetakiwa kutumia afroit.org badala
ya afroit.com? hivyo hili swali nalileta kwenu wadau kwa
majadiliano.Uzoefu unaonesha website nyingi zimekuwa zikikimbilia .com
ili kuweza kuondoa ugumu wa kukumbuka domain zenye viunganishi zaidi ya
.com
Kwa kumalizia zingatia yafuatayo
Asilani:
Usipanic!
Epuka kutumia alama za ajabu ajabu kwenye domain,kama afro!t.com .
Epuka kutumia, ’2′ukimaanisha ‘to’, ’4′ ukimaanisha ‘for’, ‘u’ ukimaanisha ‘you’.
Epuka kutumia brand names au trade marks za kampuni
nyingine(tutaongelea hili kwenye mada zijazo),sio tu unaweza
kushtakiwa,bali inaweza kukupelekea kufunikwa pindi hiyo brand nyingine
ikiwa ni kubwa na maarufu zaidi yako.
Mara zote:
Hakikisha ni rahisi kuikumbuka.
Hakikisha ni rahisi kuitamka kwa simu.
Tumia lugha rahisi
Tumia maneno yenye maana
Tumia search engine keywords. (tutaongelea siku za usoni)
Chagua domain provider mwenye uhakika. Usiwe tayari kuongopewa au kurubuniwa.
Hivyo uwanja upo wazi,ongezea orodha hizi…
No comments:
Post a Comment