Pichani ni pozi tofauti za Nana alivyo kwa sasa.
Na Imelda Mtema
MSANII wa siku nyingi wa Kundi la sanaa la maonesho la Kaole, Tausi
Chuwa‘Nana’ameibuka hivi karibuni na kudai kuwa, amefanyiwa mambo ya
kilozi na watu wanaotaka kumdhurumu nyumba yake, Risasi Mchanganyiko
limemrekodi.
Nana amesema kuwa, amejenga nyumba yake maeneo ya Kiwalani, jijini Dar lakini kuna watu wenye tamaa wanaotaka kummaliza kishirikina ili waweze kuichukua nyumba hiyo ambayo ameijenga kwa jasho lake.
“Kwa kweli ninaamini kuwa nimerogwa lakini sitapenda kuwataja wahusika walionifanyia hivyo kwa sasa, kwani hata nikiwataja hakuna anayeweza kuamini kama wanaweza kunifanyia ubaya ili nisiweze kuwa na mbele wala nyuma katika maisha yangu.
“Ndugu zangu wamenipeleka kwa waganga wakidhani miye ni kichaaa wakati si kweli, miye siyo kichaa ingawaje ninakiri kurogwa ili kuvurugiwa mambo yangu bado nina akili timamu najua kila ninachokifanya,” alisema.
Pia, msanii huyo amelalamikia kitendo cha kufungiwa ndani kwa wiki nzima ili asiweze kutoka na kuweza kufanya mambo yake ya kutafuta haki zake ili aweze kuishi na mwanaye nyumbani kwake hapo.
“Nafungiwa na ndugu zangu hata siku tatu au wiki ili nisitoke nje kwa kuaminika kuwa nimerukwa na akili kitendo ambacho sikipendi katika maisha yangu,” alisema kwa hasira Nana.

No comments:
Post a Comment