July 25 2012 Mbunge wa Kigoma
Kaskazini Zitto Kabwe alizungumza bungeni Dodoma na kusema “Makampuni ya
simu Tanzania kwa mwaka yanapata shilingi bilioni 43 kutokana na
biashara ya ringtones za nyimbo za wasanii, tulitarajia tunaponunua hizo
ringtone wasanii wetu watafaidi lakini asilimia 80 ya fedha hizo
inakwenda kwa kampuni ya simu alafu asilimia saba tu ndio inakwenda kwa
msanii”
Siku sita baada ya hii kauli
wasanii mbalimbali walioungana wakiwemo wa Bongo fleva, Gospel na Dance
na kutangaza kusimamisha mikataba ya mauzo ya nyimbo zao kama ringtones
kwenye makampuni ya simu.
Staa wa single ya ‘Ameen’ Mwana
Fa ni miongoni mwa wasanii waliofanya hivyo pia, ambapo leo ameamplfy
kwamba huwa hapendelei kutaja mapato yake hadharani lakini amekubali
kutaja ili kutoa picha kamili ya kile wasanii wanachokipata kwenye mauzo
ya ringtones.
Amesema hamna chochote ambacho
amewahi kukifanya cha maendeleo kutokana na pesa ya mauzo ya nyimbo zake
kama ringtones wakati nyimbo zake nyingi zilizohit aliziuza kama
ringtone pia, na kutolea mfano Smash hit ya ‘Yalaiti’ aliyofanya na
Linah ambapo kwenye mauzo ya ringtone kwenye miezi mitatu alipata
shilingi kama laki tatu.
Fa alitaja pia sehemu ya list
ya wasanii walioungana na kusimamisha mikataba yao ya hayo mauzo ya
ringtone na makampuni ya simu kuwa ni Profesa Jay aliekua wa kwanza, Ay,
Roma, Diamond Platnums, Fid Q na THT ambapo wamesimamisha hayo mauzo
mpaka maamuzi ya kulipwa vizuri yatakapofanywa na makampuni ya simu.
Kwenye Press release ya kuuvunja huo mkataba, wasanii wameandika “Kwa
ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel,
Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agizo kwenu la
kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na
Callertunes katika mitandao ya simu na kufuta mkataba tuliosaini kati
yetu sisi Wasanii na Kampuni mpaka hapo tutakapokaa sisi kama wasanii,
nyinyi kama wasambazaji wa muziki wetu, pamoja na Mitandao ya simu ili
kuzungumzia namna mpya ya sisi na nyinyi kufanya kazi.
“Sababu ya kusimamisha na
kufuta mikataba na wanaofanya biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja
kampuni husika kushindwa kuweka wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja
na kutolipa katika muda husika kama ilivyoanishwa katika mikataba
husika”
Mpaka July 31 2012 jioni ni wasanii 153 walikuwa wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea
No comments:
Post a Comment