Kwenye kipindi cha maswali na
majibu Aug 1 2012 bungeni Naibu waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba
alijibu kuhusu hasara ya ajali ya ndege ya shirika la ndege Tanzania
iliyotokea Kigoma tarehe 9 April 2012 pamoja na uhaba wa ndege kwa
sababu shirika la ndege Tanzania linazo ndege mbili tu.
Tizeba amesema “ni kweli kwa
sasa shirika la Ndege Tanzania linazo ndege mbili tu, moja ikiwa
inamilikiwa na shirika lenyewe na nyingine ya kukodi, historia ya hili
shirika nadhani inafahamika kwa sababu baada ya kuingia ubia wa aina
mbalimbali huduma zilidorora na likaserereka kuelekea huko”
Kuhusu hasara iliyojitokeza
kwenye ajali Kigoma, Naibu Tizeba amesema “ndege inayo gharama yake na
ndio maana baada ya kupata ile ajali tulilipwa bima kiasi cha shilingi
bilioni 10.2 lakini hasara iliyopatikana ilikua kwenye biashara hasaa na
sio gharama ya ndege yenyewe.
Gharama iliyopatikana kutokana
na kulazimika kuwalipia hoteli abiria walioshindwa kusafiri kutokana na
ajali hiyo imetajwa kwamba ni milioni 499 ambayo ilitumika kulipia
hoteli pamoja na mambo mengine.
Tayari imetangazwa na waziri wa Uchukuzi kwamba pesa hiyo ya bima itatumika kununua ndege mbili mpya.
No comments:
Post a Comment