Mpatanishi wa Umoja wa Afrika,
Thabo Mbeki, ametangaza mapatano baina ya Sudan na Sdudan Kusini kuhusu
malipo ya mapato ya mafuta baada ya mzozo wa miezi kadhaa, ambao
ulikaribia kuingiza mataifa hayo mawili vitani.
Bwana Mbeki aliwaambia waandishi wa habari
katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, kwamba maswala yote yaliyokuwa
yamebaki, sasa yametatuliwa, lakini hakutoa maelezo zaidi.
Sudan na jirani yake hawakusema kitu hadi sasa.
Sudan Kusini ilisitisha usafirishaji wa mafuta
kupitia Sudan mwezi wa Januari, kufuatia mzozo kuhusu ada iliyokuwa
ikitozwa na serikali ya Khartoum.
No comments:
Post a Comment