Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Bi Hillary Clinton amezitaka Sudan na Sudan Kusini kumaliza uhasama baina yao.
Akizungumza mjini Juba amesema uhasama ambayo ulizifanya nchi hizo mbili zikaribie vita hazifai kwa nchi ambazo ni jirani.
Bi Clinton ndiye afisa wa kwanza wa ngazi ya juu zaidi wa Marekani kuzuru nchi hiyo tangu ijipatie uhuru Julai mwaka jana.
Makataa iliyowekwa na Umoja wa Mataifa ya kutaka
nchi hizo mbili kumalizi tofauti zao kuhusu malipo ya upitishaji wa
mafuta ilikamilika jana.
Sudan Kusini ndio nchi ya pili ambayo Bi Clinton anazuru katika ziara yake ya mataifa saba ya bara Afrika.
Waziri huyo aliwasili Juba majira ya alasiri akipitia Senegal akitokea ,Uganda.
"Ijapo Sudan na Sudan Kusini sasa ni nchi
tofauti lakini maendeleo yao yanategemea uhusiano kati yao," alisema
baada ya kukutana na Rais Salva Kiir was Sudan Kusini.
"Ni jambo la dharura kwa nchi hizi mbili,
Kaskazini na Kusini, kuendelea kujadiliana ili muafaka kuhusu utata
baina yao uweze kupatikana.
"Kila moja ya nchi hizo ni sharti zilegeze misimamo yao iliklupunguza uhasama kati yao"
Matamshi ya Bi Clinton akiwa Senegal yaliolaumu
sera za serikali ya China kuhusu sera zake barani afrika matamshi yake
yameshutumiwa na vyombo vya serikali ya China.
Katika taarifa yake mjini Dakar Bi Clinton
alisema Marekani inazingatia zaidi mfumo wa uhusiao wenye manufaa kulko
ule wa kunyonya raslmali.
No comments:
Post a Comment