Wachunguzi wa Umoja wa
Mataifa nchini Syria wamesema kuwa shambulio lilofanywa na serikali siku
ya Alhamisi katika kijiji cha Tremseh inaelekea lililenga wanajeshi
walioasi na wanaharakati wa upinzani.
Wachunguzi hao walisema baada ya kuzuru kijiji hicho, kwamba jeshi lilitumia silaha nzito, kama mizinga, katika shambulio hilo.
Damu ilitapakaa kwenye nyumba zilizolengwa, na nyumba tano ziliteketezwa.
Upinzani ulisema mauaji hayo yalikuwa makubwa
ambapo watu zaidi ya 200 waliuwawa, lakini hawakutoa ushahidi thabiti
kuwa raia wengi wasiokuwa na silaha ndio waliouwawa.
Wachunguzi hao watarudi tena leo kwenye kijiji hicho kuendelea na kazi yao.
No comments:
Post a Comment