Mabingwa wa CAF MAS Fez nje ya michuano!
Mabingwa watetezi wa Kombe la shirikisho barani Afrika, klabu ya MAS Fes kutoka Morocco
ilimaliza mechi bila wachezaji wake wanne na kuondolewa katika kinyanganyiro hicho na Athletic Club Leopards ya Congo Brazzaville 2-0 mjini Brazaville.
ilimaliza mechi bila wachezaji wake wanne na kuondolewa katika kinyanganyiro hicho na Athletic Club Leopards ya Congo Brazzaville 2-0 mjini Brazaville.
Klabu ya MAS iliyoiondoa Club Africain ya
Tunisia kwa matuta mwaka jana kuwa klabu ya tatu kutoka Morocco kushinda
Kombe hilo, ilimpoteza mcheza kiungo Rachid Dahmani aliyeonyeshwa kadi
nyekundu kabla ya Bienvenu Kombo kufunga bao la Wacongo la kwanza mnamo
dakika ya 40.
Refa
kutoka Anngola alilazimika kuwafurusha mabeki wawili Omar Ennamsaoui na
Said Hammouni katika dakika tano za mwisho kabla ya beki mwingine
Younes Lyousfi naye kuona nyekundu katika dakika za majeruhi.
Licha ya upungufu huo klabu ya MAS iliweza
kudhibiti hali ya mambo hadi Yapo Guolelida kufunga mkwaju wa peneti na
kuiwezesha klabu yake kuingia hatua ya robo fainali.
Klabu hii Leopards kutoka mji wa Dolisie ulio
magharibi mwa nchi iliweza kuvuka kipigo cha duru ya kwanza kwa kuinyuka
klabu ya Tunisia CSS 2-0 nyumbani kwao Sfax.
Wacongo hao pia waliiondoa klabu nyingine kutoka
Jamhuri ya Afrika ya kati Tempete Mocaf na Heartland ya Nigeria kwenye
michuano mingine ya kufuzu kuingia hatua ya makundi, ambapo washiriki
watajishindia kitita cha dola za Marekani 165,000 zawadi.
Klabu nyingine Black Leopards ya Afrika ya
kusini nayo iliwashangaza wengi bila kutarajiwa kwa kuingia duru ya tatu
ingawa ililazimishwa suluhu 0-0 dhidi ya Al Merreikh ya Sudan, washindi
wa mwaka 2007 licha ya kunyukwa 3-2 mjini Omdurman majuma mawili kabla.
Watani wa Mereikh katika Ligi ya nyumbani Al
Hilal pia walipiga hatua kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Cercle Bamako
nchini Mali kupitia bao la kipindi cha kwanza lililofungwa na Mudathir
Eltaib baada ya mabao mawili ya mchuano wa kwanza.
Vilabu vingine vya Mali navyo vilinusurika
ambapo Stade Malien ililazimisha sare ya 1-1 na COD Meknes ya Morocco
nyumbani kwao na hivyo kusonga mbele kwa jumla ya bao 4-1.
Djoliba nayo ilipenya kupitia matuta baada ya kupoteza mchuano wa kwanza 2-0 nyumbani kwa Club Africain mjini Tunis.
Abdelali Essamlali aliipa klabu yake Meknes
matumaini kwa bao mnamo dakika ya 21, lakini Lamine Diawara akarudisha
kabla ya mapumziko.
Hamzi Agrebi aliongezea matumaini ya Africain
kwa bao la pili lakini Haj Massaoud kurudisha kupitia mkwaju wa peneti
ikiwa zimesalia dakika saba. Hatimaye ilibidi mchuano uamuliwe kwa
matuta ambapo Djoliba ilishinda kwa 4-3.
Klabu pekee ya Morocco iliyonusurika na Wydad
Casablanca, iliyotoa suluhu dhidi ya AFAD Djekanou ya Ivory Coast na
kupiga hatua kutokana na ushindi wa ugenini.
No comments:
Post a Comment