Huku ikiwa imesalia wiki mbili
kuanza kwa michezo ya olimpiki, serikali ya uingereza imekuwa ikitetea
vikali mipango yake ya usalama baada ya kuongeza maelfu ya wanajeshi
kulinda maeneo ya michezo hiyo.
Waziri wa mambo ya ndani wa uingereza Theresa
May aliliambia bunge kuwa usalama katika maeneo ya michezo hiyo
umepangwa vilivyo lakini akasema kuwa kumezuka hofu kuhusiana na uwezo
wa kampuni ya ulinzi ya G4S kuwafunza wafanyikazi tosha.
Zaidi ya wanajeshi elfu tatu mia tano wameitwa na kufikisha alfu kumi na saba walinzi katika mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment