Mashirika ya kuto misaada katika kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani , Dadaab yamesema yamepungukiwa na pesa.
Makundi hayo yameonya kuwa ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa basi hali ya maisha ya maelfu ya wakimbizi yatakuwa hatarini.
Idadi ya wakimbizi katika kambi hiyo ya Dadaab
ambayo iko karibu na mpaka wa Kenya na Somali imeongezeka kwa zaidi ya
thuluthi moja katika kipindi cha mwaka mmoja.
Kambi hiyo kwa sasa ni hifadhi ya zaidi ya wakimbizi nusu milioni.
Mwaka jana , maelfu ya Wasomali walimiminika
katika kambi hiyo kutokana na hali ya ukame, njaa pamoja na vita
viliovyokuwa vikiathiri nchi yao.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya Dunia Mike
Wooldridge anasema kwamba wakati huu bado maelfu ya wakimbizi wanaishi
katika vyandarua ambavyo vinazidi kuchakaa na kuharibika kutokan na hali
mbaya ya ya anga.
Mashirika hayo ya kutoa misaada inasema wakimbi
wapatao 30,000 wanahitaji makao lakini kwa wakati huu kuna pesa za
kusaidia wakimbizi 4,000 peke yake.
Maji safi kwa wakimbizi karibu 50,000 pia yanahitajika kwa haraka ili kuzuia wasipate maradhi ambukizi kama vile kipindupindu.
Wakati huo huo mashirika hayo yamesema kuna haja ya suluhisho la kudumu kutafutwa.
No comments:
Post a Comment