Askofu mpya kabisa kutawazwa
imearifiwa kuwa anashikiliwa na mamlaka ya Uchina baada ya kutangaza
kuwa anajiuzulu kutoka Kanisa Katoliki linalokubalika na Mamlaka ya
Uchina.
Thaddeus Ma Daqin, Askofu wa Shanghai,
alitangaza hatua yake ya kujiuzulu kutoka Chama kijulikanacho kama China
Patriotic Association (CPA) siku ile ambapo alitawazwa wiki iliyopita.
Duru za Kanisa Katolika na vyanzo vingine vya
kidini vimesema kuwa kiongozi huyo wa dini anashikiliwa ndani ya
Seminariyo moja karibu na Shanghai.
Kwa mda mrefu kumekuwepo hali ya kutofahamiana baina ya Uchina na Vatican.
Vatican, iliyomteuwa Askofu Ma, haitambui chama
cha CPA kinachokinzana na Kanisa Katoliki na Kanisa Katoliki nchini
Uchina halitambui Mamlaka ya Papa.
Waumini wanaokadiriwa kutimu milioni 10 wa huko
Uchina wamegawika kati ya wafuasi wa Papa na upande wa pili ukikubaliana
na kundi la Chinese Patriotic Catholic Association (CPA).
Taarifa zinasema kuwa Askofu Ma aliuambia ummati
wa watu 1,000 kuwa ameamua kujiuzulu ili awezew kushughulikia majukumu
yake mapya. Tangazo lake hilo lilifuatiwa na makofi ya waumini , kwa
mujibu wa habari za gazeti linalochapishwa huko HongKong la South China
Morning Post.
Lakini wadadisi wanasema kuwa hatua hio
ilionekana na wakuu wa Uchina kama kejeli na kudharau udhibiti wa Dola
la Uchina juu ya viongozi wa Kanisa Katoliki na wengine.
No comments:
Post a Comment