Bunge la Misri limerejelea vikao
vyake mapema hii leo kufuatia agizo lililotolewa na rais mpya wa nchi
hiyo Mohamed Mosri, lakini kikao hicho kikaahirishwa baada ya muda
mfupi.
Bunge hilo lilirejelea vikao vyake na kukiuka
agizo lililotolewa na Baraza la Kijeshi linalotawala, ambalo lilivunja
bunge hilo kufuatia uamuzi wa mahakama ya kikatiba.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya
habari, mapema hii leo, Baraza hilo la Kijeshi lilisema kuwa ni sharti
raia wote wa nchi hiyo waheshimu uamuzi uliotolewa na mahakama ya
kikatiba.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo, anasema malumbano
makali yanaendelea kutokota kati ya rais Morsi na maafisa waandamizi wa
jeshi. Hata hivyo rais Morsi alijitokeza hiyo jana katika hafla rasmi ya
serikali akiandamana na maafisa kadhaa waandamizi wa Baraza hilo la
Kijeshi.
No comments:
Post a Comment