TANGAZO KWA MADAKTARI WA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI...!!!
Uongozi
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili unawatangazia Madaktari wote ambao
hawafiki kazini kuwa wanatakiwa kurudi kazini mara moja kwa
kujiorodhesha majina yao kwa wakuu wao wa Idara.
Aidha,
tangazo hili pia linawahusu Madaktari wote wanaokuja kazini lakini
hawafanyi kazi, nao wajiorodheshe kwa wakuu wao wa Idara.
Wakuu
wote wa Idara wanatakiwa kuwaorodhesha Madaktari wote watakaofika
kazini kuanzia leo (2/Julai/2012) na kuhakikisha wanafanya kazi kwa
mujibu wa sheria, kanuni, na taratibu zilizopo.
Zoezi hili litafungwa kesho tarehe 3 Julai 2012 saa tatu asubuhi.
Tangazo hili haliwahusu Madaktari walio katika Mafunzo kwa Vitendo (Interns).
Dr. Marina Njelekela,
Mkurugenzi Mtendaji
Saa 06:00 Mchana
Nakala: Wakurugenzi - Kwa usimamizi
No comments:
Post a Comment