SIRI BANK YA TWIGA BANCORP KUPEWA TUZO GENEVA YAANIKWA...!!!
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp Limited, Hussein Mbululo (kulia)
akifafanua jambo juu ya Tuzo ya Dhahabu waliyo ipata kutoka Geneva Uswis
kwa Ubora wa huduma zao, kwa waandishi wa Habari waliotembelea banda la
Benki hiyo katika maonesho ya kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam
yanayoendelea katika viwanja vya JK Nyerere maarufu Saba Saba barabara
ya Kilwa. Pamoja ni wafanyakazi wa Benki hiyo waliopo viwanjanani hapo.
SIKU chache
baada ya kupokea Tuzo ya dhahabu ya Kimataifa ya utoaji bora wa huduma,
Benki inayomilikiwa na Serikali ya Twiga Bancorp, imeweka hadharani siri
ya kupewa tuzo hiyo inayojulikana kama Century International Gold
Quality ERA.
Benki ya
Twiga Bancorp ilikabidhiwa tuzo hiyo karibuni na Kampuni ya Kimataifa ya
Business Initiative Directions jijini Geneva Uswis.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Hussein Mbululo,
alisema huduma ya moneygram inayowezesha Watanzania na watu wa mataifa
mengine kutuma fedha nje kwa dakika chache imechangia kuiwezesha benki
hiyo kushinda tuzo hiyo.
Tuzo hiyo
kwa Benki ya Twiga Bancorp imekuja siku chache baada ya Serikali kupitia
kwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. William Mgimwa kuliambia Bunge
kwamba Serikali ipo mbioni kuziongezea mtaji benki zake ikiwemo Benki ya
Twiga ili kuziwezesha kuboresha huduma zake. Benki nyingine ni Benki ya
Wanawake (TWB), Benki ya Posta (TPB) na Benki ya Rasilimali (TIB).
Mbululo
alisema huduma nyingine iliyoiwezesha benki hiyo kushinda tuzo hiyo ni
utoaji wa mikopo kwa wafanyakazi bila kuwalazimu wafanyakazi hao kuwa na
akaunti katika Benki ya Twiga hatua ambayo imewezesha wafanyakazi nchi
nzima hata mahali kusiko na benki hiyo kunufaika na mikopo hiyo.
“Walieleza
kuridhishwa na huduma zetu kufikia kiwango cha ubora wa juu lakini pia
walieleza kuridhishwa na ubunifu tunaoendelea kuufanya katika kuboresha
huduma za kibenki nchini ukilinganisha na benki nyingine.
Kupitia
huduma za Money gram mtu anaweza kumtumia fedha za ada au dawa kwa
mwenzake aliyepo Uingereza au Marekani na akaweza kuzipata ndani ya
dakika tano tu jambo ambalo limewavuta watu wengi kutumia benki yetu,”
alisema Mbululo.
Alisema
benki hiyo pia imetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Benki Kata za
Jamii (VICOBA) katika maeneo mbalimbali hapa nchini hatua ambayo
imewezesha kupewa nishani ya kuwa mlezi bora wa VICOBA nchini na kupewa
tuzo.Hadi sasa Benki hiyo inahudumia vikundi zaidi ya 150 vya VICOBA.
Alisema
benki hiyo inayoendelea kujitanua kwa kufungua tawi moja mkoani kila
mwaka, hivi karibuni itafungua tawi jipya mkoani Dodoma na hivyo
kuifanya kuwa na matawi Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Dodoma, huku
tawi la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, likiendelea
kuvunja rekodi ya kufunguliwa kwa saa 24 kwa siku zote saba za wiki.
Alisema
mtandao wa huduma kwa benki hiyo umeimarika kutokana na kadi zake za ATM
kuweza kuunganishwa na Mtandao wa Umoja wenye kuzihusisha benki zaidi
ya 24, zikiwa na mtandao wa zaidi ya ATM 160 nchi nzima.
Kuhusu mtaji
utakaongezwa na serikali kwa benki hiyo, Mbululo alisema fedha hizo
zitasaidia kuboresha huduma za benki hiyo kwa kuwezesha kujenga matawi
mapya, kununua mashine na kununua kompyuta na vifaa vyake ili kutanua
zaidi huduma zake na kuwezesha kuwafikia wananchi wengi.
Afisa
Mwandamizi, Mwendeshaji, Lydia Matembele akitoa maelezo kwa vijana
waliotembelea banda lao katika maonesho ya Kimaifa ya Biashara maarufu
saba saba .
Banda la Twiga Bank lipo kando ya lango kuu la Kuingilia Karume Hall.
Benki ya
Twiga Bancorp inatoa huduma ya kuweka na kuchukua fedha dirishanai au
katika ATM yake iliyopo viwanja vya Sabasaba kama mmoja wa wateja wa
Umoja Switch anavyofanya.
Mkuu wa Uendeshaji Richard Kombole (kulia)akizungumza na mteja nje ya Banda lao
Afisa
Mwandamizi, Mwendeshaji, Lydia Matembele akimsikiliza Mfanya Biashara,
Yahia Idriss wa Kampuni ya Giad Sewedy Cables ya Nchini Sudan alipofika
kupata huduma ya kubadilishiwa fedha katika Banda hilo la Maonesho
linalofanya huduma kamili za Kibenki.
No comments:
Post a Comment