Amesema Moja kati ya ishu anazopiga ni “kununua nyumba na kuziuza,
kukodisha, pia kununua mashamba na kuyauza huko Uganda, na kuna biashara
nyingine nimeianza juzi juzi ya CHAMELEONE MOBILE, nilikwenda China na
kuungana na kampuni moja ya China wakatengeneza simu inaitwa
CHAMELEONE, hiyo ni moja kati ya kazi zangu kubwa… watu wanazinunua sana
nyumbani Uganda, ni handset ambayo unaweza kuweka line ya mtandao
wowote”
Kwenye line ya mwisho ChameleonE kasema “hii ni kujaribu kufikiria
nje ya box pamoja na kujaribu kufanya mipango uliyokua nayo kichwani, na
bado naendelea baada ya hizo simu nataka kutengeneza vitu vingi zaidi..
nataka jamii yangu inikumbuke kwa nilichowafanyia”
Hayo ndio aliyoyasema Staa wa muziki Jose Chameleone wa Uganda nchi
inayotajwa kuwa na wasanii wanaoongoza kwa kuwa na pesa nyingi kuliko
nchi yeyote Afrika Mashariki.
Tayari mpaka sasa kuna baadhi ya mastaa ambao wamejaribu kupiga dealz
nyingine mbali na muziki akiwemo Lady JayDee ambae anamiliki Mgahawa,
Jua Cali wa Kenya alitangaza kuanza kutengeneza headphone kama za Beat
by Dre, Profesa Jay nae alitangaza kwamba ndoto zake hazipo kwenye
magari ya kifahari sasa hivi au anasa nyingine, anajipanga kwa ajili ya
kuinvest kwenye ardhi for now.
No comments:
Post a Comment