Nahitaji
ufahamu kwamba hii nafasi nimeitoa rasmi leo kwa sababu ya ishu ambayo
imekuzwa na mitandao ya kijamii inayotumiwa sana na watanzania wengi
muda mfupi baada ya kamishna msaidizi wa polisi Ahmed Msangi kumtembelea
hospitali kiongozi wa Madaktari Dr Ulimboka Steve ambapo mistari kadhaa
imesambazwa kwenye mitandao hiyo ikimuhusu Kamanda Msangi.
Mistari ambayo ni maarufu ambayo inadaiwa kutolewa na mtu anaedai
alisikia kila kitu ni kwamba Dr Ulimboka alipomuona tu Kamanda Msangi
amekwenda kumtembelea hospitalini, alianza kumwambia ampe viatu vyake
pamoja na simu yake, ikimaanisha kwamba Ahmed Msangi alikuepo wakati Dr
Ulimboka akifanyiwa huo ukatili.
Exclusive na millardayo.com Msangi amesema “hata mimi hizo habari
nimezisikia na kuzisoma kwenye mitandao na msg zinazotumwa, kiukweli
taarifa hizo zote sio za kweli kuna mtu tu amekaa na kuona atunge kitu
labda kwa malengo yake mwenyewe, ni kweli nilikwenda kumtembelea
hospitalini na nilipitia kwa mkurugenzi wa Moi na ndio tukaambatana
pamoja kwenda wodini kumuona Ulimboka, ananifahamu na mara nyingi
tunakutana hata kwenye sehemu za kufurahi hivyo akanihadhia jinsi
ilivyokua na nikamuuliza maswali kwa ajili ya upelelezi”
Haijawezekana kumpata dr Ulimboka sasa hivi kwa sababu ya taratibu za
hospitali, lakini nitaitumia nafasi kwa saa chache zijazo… mpango
ukifanikiwa ripoti utaipata manake neno lake yeye ni muhimu sana kwenye
hii ishu.
No comments:
Post a Comment