MWANACHUO WA CHUO CHA UALIMU ST. AGREY JIJINI MBEYA AUAWA BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA BODABODA
Vedasto Pius baada ya kupigwa vibaya na wananchi.
Pikipiki inayodaiwa kuibiwa na Vedasto Pius.
Kitambuliso cha Chuo cha Vedasto Pius.
Mwananchuo mmoja kutoka Chuo cha Ualimu cha ST Aggrey kilichopo Uyole
jijini Mbeya, anasadikiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na wananchi
wenye hasira kali katika maeneo ya Isanga kwa tuhuma za kuiba pikipiki
ya kusafirishia abiria maarufu kama bodaboda.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo PRAY GOD MGONJA amemtaja mtuhumiwa
huyo kuwa ni VEDASTO PIUS anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25
mpaka 30.
Mgonja amesema tukio hilo lilitokea mnamo Julai 2 mwaka huu majira ya
saa 8 mchana katika daraja lililopo karibu na hotel ya Rift Valley
barabara ya kuelekea Isanga, Jijini Mbeya.
Amesema mtuhumiwa amekumbwa na mkasa huo baada ya tuhuma za kuiba
pikipiki yenye No T 438 BZU aina ya T-BETTER mali ya JOSEPH KAPASI (23)
mkazi wa Ilomba jijini hapa.
Kwa upande wake mmiliki wa pikipiki hiyo JOSEPH KAPASI amesema
aliombwa kumfundisha mtuhumiwa huyo na baadae mtuhumiwa alipoanza
kuendesha vizuri alitokomea na pikipiki hiyo. Baada ya tukio hilo
mtuhumiwa alikutwa eneo la Isanga akielekea barabara ya Chunya akiwa na
pikipiki hiyo ndipo alipoanza kupewa kipigo na wananchi wenye hasira
kali mpka mauti kumfika.
No comments:
Post a Comment