MPAMBANO WA NGUMI UWANJA WA TAIFA: WEMA NIMEKWIVA
MSANII wa filamu, Wema Sepetu ambaye
anatarajiwa kuchapana makonde na Jacqueline Wolper katika pambano la
utangulizi kesho, amesema sasa amekwiva na yuko fiti kutokana na mazoezi
ambayo anapewa na kocha wake Rashidi Matumla.
Akizunguza na gazeti hili jana, Wema
alisema ametumia muda mwingi katika mazoezi hivyo kesho ni lazima
atampiga Wolper kwa ‘knock out’.
“Kwa kweli nimejifua vilivyo lengo likiwa ni kuhakikisha naweka historia kesho ya kumchakaza Wolper, kwa nilivyo fiti sidhani kama atafikisha raundi ya pili,” alisema Wema.
Wakati Wema akisema hayo, Wolper amejigamba kwa kusema: “Wema ajiandae tu kwa kipigo, ameshasema mengi ila mimi siku hiyo nataka nimfundishe adabu. Nitamvuruga, nitampiga na kwa uzito wa ngumi nitakazomtupia asipotoka manundu labda awe amechanjia.”
Warembo hao wamesema kuwa wanapigana kumaliza ubishi wa muda mrefu, vilevile kuchangia fedha Mamlaka ya Elimu Tanzania ili kuwasaidia wanafunzi wa kike kupata mabweni na kusoma katika mazingira mazuri.
Mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto amesema kuwa Wolper na Wema kila mmoja anatamba kumpiga mwenzake, hivyo akataka mashabiki wao kuhudhuria Uwanja wa Taifa ili kumuona mbabe kati ya wawili hao.
“Tumekubaliana kwa kufuata misingi yote. Wolper na Wema wameridhia kupambana ili kumaliza ubishi na kuchangia elimu,” alisema Luqman na kuongeza:
“Wolper na Wema wataingia uwanjani kwa helikopta. Tunatambua thamani ya Wema na Wolper kijamii, kwa hiyo hatutaki wapitie njia ambazo zitawafanya watoe kisingizio. Tutawaingiza kwa helikopta, kila mtu na ya kwake ili watakapokuwa wanaingia, uwanja mzima ushuhudie.”
Luqman aliendelea kusema kuwa pambano la Wema na Wolper litakuwa la utangulizi, kabla ya mabondia wakubwa nchini, wenye rekodi nzito, Japhet Kaseba na Francis Cheka kupambana kwenye pambano la kumaliza ubishi.
“Kama nilivyokwishasema kabla, siku ya Tamasha la Usiku wa Matumaini ni nzito. Matukio ni mengi, vilevile kutakuwa na mechi ya wabunge Simba na Yanga, Bongo Fleva dhidi ya Bongo Movie, bila kusahau siku hiyo tutajua mkali wa steji ni nani kati ya Jose Chameleone wa Uganda na Diamond Platnamz wa Tanzania.
“Kutakuwa na shoo nyingine kali kutoka kwa Roma, Chidi Benz, Juma Nature, Pah One, FM Academia, East African Melody na wengine wengi,” alisema.

No comments:
Post a Comment