Mwanariadha aliyetumainiwa
kushinda medali ya dhahabu kwa kasi yake na uhodari katika mbio za mita
1500 Mariem Alaoui Selsouli hatoshiriki mashindano ya Olimpiki kwa
kupatikana kua alitumia dawa ya kuongezea nguvu mwilini.
Selsouli mwenye umri wa miaka 28 alishinda
medali ya fedha kwenye mashindano ya Dunia mwaka huu alipatikana kutumia
dawa iliyopigwa marufuku aina ya furosemid kupitia vipimo
vilivyochukuliwa tareh 6 Julai mjini Paris.
Mariam Alaoui amewahi kufungiwa kwa kutumia dawa za kuongezea nguvu mwilini na safari hii huenda akafungiwa maisha.
Katika taarifa yake, Shirikisho la michezo ya
Riadha duniani IAAF limetangaza kuwa aina ya dawa ya furosemide
iligundulika mwilini mwa mkimbiaji huyo.
"Alaoui Selsouli binafsi aliondoa haki yake ya
ukaguzi wa pili na kutokana na hilo amesimamishwa kutoshiriki mashindano
yote ya riadha.
Kulingana na Sheria za IAAF bado mwa\nariadha
huyo ana haki ya kuomba kesi isikilizwe ambapo chama cha riadha cha
Morocco kinatakiwa kuhudhuria.
No comments:
Post a Comment